WACHIMBAJI WADOGO KAHAMA WAPATIWA ELIMU YA USIMAMIZI NA USALAMA MIGODINI.
Picha ya pamoja ya viongozi wa wachimbaji wadogo na maafisa kutoka tume ya madini nchini wakati wa mafunzo ya usimamizi na usalama migodini yaliyofanyika wilaya ya kahama leo hii.
Winnifrida Mrema meneja ukaguzi wa migodi kutoka tume ya madini nchini akichukua taarifa wakati wa kikao.
Wachimbaji wa madini kutoka wilaya ya Kahama walioshiriki mafunzo ya usimamizi na usalama migodini kutoka tume ya madini Tanzania.
Kamanda wa jeshi la zimamoto wilaya ya Kahama Inspector Hanafi
Nkilindi akielezea namna ya zoezi la usalama na uokoaji mgodini.
Kaimu mkurugenzi ukaguzi migodini na Mazingira Henry Mditi akiongea
na wachimbaji wadogo kuhusu Sheria na kanuni za usalama ,usimamizi wa
mgodi,uteuzi na mamlaka ya meneja mgodini.
Joseph Nalimi -Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo wilaya ya Kahama akizungumza juu wakati wa mafunzo ya usimamizi na usalama kwa wachimbaji wadogo.
Katibu Tawala wilaya ya Kahama,Timothy Ndanya akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Kahama.
Na Neema Sawaka,
WACHIMBAJI
wadogo na viongozi wanaosimamia migodi kwa mkoa wa kimadini Kahama
wamepatiwa elimu juu ya usimamizi wa mgodi ,Sheria na kanuni za
usalama ,uteuzi na mamlaka ya meneja mgodini .
Mafunzo
hayo yametolewa leo machi 11,2022 na wataalamu kutoka tume ya madini nchini ambapo
mgeni rasmi akiwa katibu tawala wilaya ya Kahama Timothy Ndanya kwa
niaba ya mkuu wa wilaya hiyo Festo Kiswaga .
Dkt
Anorld Gesesa mkurugenzi wa huduma za sheria kutoka tume ya madini
amesema kuwa Sheria ya madini ya mwaka 2010 iliyofanyiwa marekebisho
yake mwaka 2017 na kanuni zake nyingi ambazo wachimbaji wadogo
wamekuwa hawazifuati na kuwasababishia madhara endapo wakizifuata
wangeweza kuepuka madhara yote yanayotokea kwa watu.
Winnifrida
Mrema ambaye ni meneja ukaguzi wa migodi kutoka tume ya madini
amesema kuwa wachimbaji wamekuwa wakifanya kazi za mazoea bila
kuzingatia sheria za usalama mahali pa kazi ambapo shughuli za mgodini
maeneo siyo salama hivyo yameweza kusababisha vifo .
"Hatutaki
maeneo ya uchimbaji yasiwe salama tunataka yawe salama na wachimbaji
wafanye kazi kwenye maeneo salama na wanaosimamia wanatakiwa wazingatie
Sheria ili kuweza kuwavusha salama na mkakati wa kusanifu mgodi
watumike wataalamu waziri ili kubuni muundo na usanifu katika eneo
husika" amesema Mrema.
Mhandisi Henry Mditi Kaimu mkurugenzi ukaguzi migodini na mazingira kutoka
tume ya madini amesema kuwa uteuzi na mamlaka ya mameneja mgodini ni
upo kisheria na mgodi haupaswi kufanya kazi zaidi ya siku saba bila
kuwa na meneja mgodi.
"Sheria
ya madini sura ya 123 na kanuni za uchimbaji mdogo za mwaka 2010
zimeainisha mambo ya msingi ya kuzingatia katika usimamizi wa
afya,usalama na utunzaji wa mazingira kabla ya kuanza uchimbaji,wakati
wa uchimbaji na baada ya uchimbaji."amesema mhandisi Mditi.
Ofisa
madini mkazi wa mkoa wa kimadini Kahama Jeremiah Hango amesema kuwa
mkoa una jumla ya leseni za uchimbaji mdogo 592 ambapo leseni za
utafutaji madini zipo leseni 65 Kati ya hizo zipo baadhi katika hatua
ya awali.
Mgeni rasmi
katibu tawala wilaya ya Kahama Timothy Ndanya amesema kuwa changamoto
kubwa iliyopo kwa wachimbaji hawa ni kuripotiwa wizi wa carbon ambapo
mtu akibainika uongozi wa wilaya hautamvumilia kumfutia leseni na wengi
wao wamekuwa hawafuati sheria na taratibu zilizopo.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464