BEI YA MAFUTA PETROLI YAPAA HADI SH. 2,861


Wakati Serikali ikitangaza kurejesha Sh100 katika mafuta, watumiaji wa nishati hiyo watalazimika kufunga mkanda kutokana na bei kuendelea kupa.


Bei ya nishati hiyo inapanda wakati wananchi wakilalamika kupaa kwa bei za bidhaa mbalimbali za vyakula hasa wakati huu wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Hata hivyo, vita vya Russia na Ukraine ambavyo vimedumu kwa zaidi ya mwezi sasa navyo vinatajwa kupandisha bei ya nidhati hiyo kwenye soko la dunia. Russia ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa mafuta dunia.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Jumanne Aprili 5, 2022 Mkurugenzi wa Petroli wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Gerald Maganga amesema kuanzia kesho Jumatano, Aprili 6,2022 bei mpya ya petrol kwa mafuta yanayopokelewa kupitia Bandari ya Dar es salaam itakuwa Sh2,861 kutoka Sh 2,540 ikiwa ni ongezeko la Sh321.

SOMA HAPA ZAIDI CHANZO MWANANCHI.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464