Naibu Katibu Mkuu Bara kutoka Chadema Benson Kigaila akizungumza kwenye kikao hicho.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
CHAMA cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA), kimeitaka Serikali kuweka mikakati ya kujitegemea, pamoja kupunguza kodi kwenye bidhaa mbalimbali hasa mafuta ya Petroli, ili kuepuka ongezeko la bei za bidhaa na kuumiza wananchi.
Alisema tatizo la kupanda kwa bei za bidhaa mbalimbali hapa nchini, linatokana na nchi kutokuwa na mikakati ya kujitegemea, na kubaki kutegemea vitu vingi kutoka nje ya nchi.
"Nchi yetu ya Tanzania ina Rasilimali nyingi ambazo tunaweza kuzitumia na kuacha kutegemea kila kitu kutoka nje ya nchi, fikiria hadi ngano tunaagiza kutoka Urusi na Ukraine, bidhaa ambayo hata sisi tunaweza kulima,"alisema Kigaila.
"Ili kuepukana na mifumuko hii ya kupanda kwa bei ya bidhaa mbalimbali hapa nchini, lazima Serikali iwe na mikakati yake ya kujitegemea, na siyo kila kitu ambacho hata sisi tunaweza kukifanya tukiagize kutoka nje ya nchi," aliongeza.
Naye Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chadema John Heche, alisema Serikali pia inapaswa kuweka Sera ya kupeleka pesa kwenye kilimo na kuzalisha ngano, na kubainisha kuwa kuna Mashamba ya ngano ambayo yalianzishwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo yameshageuzwa Lanchi za watu.
Akizungumzia mfumuko wa bei za bidha hapa nchini, alisema Serikali inapaswa kupunguza kodi kwenye bidhaa mbalimbali hasa mafuta ya Petroli, ambayo alidai yana tozwa kodi takribani 19 ili kuepuka mfumuko huo wa bei ya bidhaa, na kuwapa unafuu wa maisha wananchi.
Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti Chadema Kanda ya Serengeti Gimbi Masaba, alisema ili matatizo yote hayo yaishe kwa wananchi, wanapaswa kuwa na Katiba Mpya, ambayo ndiyo itakuwa ukombozi wa maisha yao na kupata viongozi sahihi wenye kuwaletea maendeleo.
Akizungumzia Ripoti ya uchafuzi ya Mto Mara, alisema chama hicho hakikubaliani na Ripoti hiyo, na kuomba Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu Rais Muungano na Mazingira Selemani Jafo pamoja na Tume yake yote wachukuliwe hatua, kwa madai ya kudanganya umma na kutoa Ripoti isiyo sahihi na kucheza na maisha ya wananchi.
Naibu Katibu Mkuu Bara kutoka Chadema Benson Kigaila akizungumza kwenye kikao hicho.
Kaimu Mwenyekiti Chadema Kanda ya Serengeti Gimbi Masaba akizungumza kwenye kikao hicho.
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chadema John Heche akizungumza kwenye kikao hicho.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho.
Hapa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Serengeti Marwa Ryoba kupitia Chadema, akatimkia CCM, na sasa ametangaza amerudi tena Rasmi kwenye Chama chake cha Chadema.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA.