CITIZEN FOR CHANGE NA WFT-T WAFANYA KIKAO KAZI NA WADAU WA KUTOKOMEZA UKATILI MKOA WA SHINYANGA

CITIZEN FOR CHANGE NA WFT-T  WAFANYA KIKAO KAZI NA WADAU WA KUTOKOMEZA UKATILI MKOA WA SHINYANGA
Mkurugenzi mtafiti wa Shirika la Citizen for Change Dkt. Kate McAlphine akiwasilisha mada uandaji wa taarifa za matokeo ya mradi katika  kikao cha asasi zinazotekeleza mradi wa kutokomeza ukatili Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.


 Wawakilishi kutoka asasi za kiraia na serikali mkoa wa Shinyanga wakitoa maoni yao katika kikao kuhusu masuala ya ulinzi na usalama wa watoto na wanawake dhidi ya ukatili.

Mwenyekiti wa Baraza la watoto Taifa ,Nancy Kasembo akitoa maoni yake kuhusu hali ya usalama na ulinzi wa watoto.

Na mwandishi wetu,

Shirika la Citizen for Change(C4C) kwa kushirikiana na Mfuko wa Wanawake Tanzania( WFT-T) limeendesha kikao kazi na wadau wanaotekeleza mradi wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Kikao kazi hicho kimefanyika leo jumanne 12,2022 katika ukumbi wa ofisi ya Mfuko wa Wanawake Tanzania Mkoa wa Shinyaga kwa ajili ya kutathimini shughuli za utekelezaji wa mradi wa kutokomeza ukatili kwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. Wadau walioshiriki ni pamoja na ICS,Rafiki SDO,Thubutu Africa Initiative,Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,YWL,YAWE,WEADO,GCI,Jeshi la polisi  mkoa wa Shinyanga ,Redio Faraja  na Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga.

Mkurugenzi wa Mtafiti wa Shirika la Citizen for Change Dkt. Kate MCAlphine  alisema lengo la kikao hicho ni kutambua matokeo ya yaliyopatikana kwa jamii kwa  nguvu ya  wadau hao  katika utekelezaji wa shughuli zao juu ya  afua mbalimbali katika  Mpango kazi wa Taifa katika Kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake  na watoto( MTAKUWWA).

" Lengo ni kutambua matokeo yaliyopatikana katika shughuli za kutokomeza ukatili kwa wadau wanaoshirikiana na Mfuko wa Wanawake Tanzania na kubaini  changamoto zinazo kwamisha utekelezaji wa mpango kazi wa Taifa kwa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto na ule mpango kazi wa mkoa wa Shinyanga wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto".Alisema Kate

Aidha Dkt.Mc Alphine   aaliwaomba wadau hao wanao tekeleza mradi huo kuwa huru kutoa maoni yao katika mjadala wa kupokea maoni  ili kuweza kupata majibu yatakayosaidia utafiti zaidi kuhusu masuala ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Citizen for Change ni Shirika linajihusisha na masuala ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika eneo la ulinzi na usalama kwa kujikita katika utafiti kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ndani ya Tanzania.

George Nyanda ,Afisa Mradi wa Shirika la Green Community Initiative (GCI) akichangia mjadala huo ,alisema kuwa ni vema jamii ipatiwe elimu zaidi kuhusu mbinu za uwasilishaji ushahidi katika vyombo vya  mahakama Ili kufanikisha upatikanaji wa  hukumu na kutoa haki kwa  wahanga wa ukatili.
" Kuna mambo ya kitaalam yanahitajika zaidi eneo la  sheria kwa kesi za ukatili zinapokuwa ngazi ya mahakama na changamoto hizo ndo zinakwamisha.

Naye Aisha Omary ,Afisa Maendeleo kutoka Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga alisema utekelezaji wa sheria za masuala ya ukatili ni wanajamii na wadau kushirikiana pamoja  na ili kuweza kukamilisha mchakato wa kesi hizo kupatiwa hukumu mapema ili kukomesha vitendo hivyo .

Kwa upande wa dawati la jinsia mkoa wa Shinyanga Mrakibu Msaidizi Monica Sehere alisema kuwa changamoto ni wanajamii kuwa na ushirikiano hafifu wa kutotoa ushahidi kwa kwa jeshi la polisi ili kulindana ndani ya familia.

George Nyanda kutoka GCI akitoa maoni yake juu ya vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto  mkoa wa Shinyanga.
Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kutoka dawati la jinsia Monica Sehere akitoa maoni yake juu ya kazi za jeshi la polisi. 
Afisa  Maendeleo wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Aisha omary akitoa maoni yake.

KAZI ZA VIKUNDI ZIKIENDELEA







Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464