KASHWASA WAFANYA HAFLA YA KUMUAGA ALIYEKUWA MKURUGENZI WAO MHANDISI JOSHUA MGEYEKWA, DAS CHAMBI ATOA UJUMBE MZITO


Mkurugenzi Mpya wa Mamlaka ya maji (KASHWASA) Mhandisi Patrick Nzamba, (kushoto) akimkabidhi zawadi ya picha iliyochorwa sura yake Mhandisi Joshua Mgeyekwa (kulia) ambaye alikuwa Mkurugenzi wa (KASHWASA) na sasa amestaafu zawadi aliyo itoa kwa niaba ya watumishi wote wa (KASHWASA).

Mkurugenzi mpya wa Mamlaka ya maji (KASHWASA) Mhandisi Patrick Nzamba (kulia), akikata keki na Mhandisi Joshua Mgeyekwa ambaye alikuwa Mkurugenzi wa mamlaka hiyo na sasa amestaafu wakikata keki ili kufungua hafla hiyo ya kumuaga.


Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MAMLAKA ya Majisafi na usafi wa mazingira Kahama na Shinyanga (KASHWASA), ambao wanazalisha maji kutoka Ziwa Victoria na kuziuzia mamlaka nyingine maji hayo na kuwasambazia wananchi, wamefanya hafla ya kumuaga aliyekuwa Mkurugenzi wao Mhandisi Joshua Mgeyekwa ambaye amestaafu utumishi wa umma.

Hafla hiyo imefanyika jana Aprili 29 katika ukumbi wa Witesh Hotel Mjini Shinyanga, na kuhudhuliwa na watu mbalimbali wakiwamo viongozi wa Serikali, Taasisi, wadau wa maji, watumishi wa mamlaka za maji, huku mgeni Rasmi akiwa Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema.

Chambi akizungumza kwenye hafla hiyo, aliwataka watumishi wa mamlaka hiyo ya maji KASHWASA, kuwa wanyenyekevu, kufanya kazi kwa umoja, uadilifu, bidii, na kumtanguliza Mungu, ili kufikia malengo yao katika utendaji kazi na kutoa huduma stahiki ya maji.

Alisema wakizingatia mambo yote hayo, hawatakwama katika utendaji wao kazi, na kuyaenzi kwa vitendo yale ambayo ameyaacha aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo ya Maji (KASHWASA)Mhandisi Joshua Mgeyekwa.

Naye Mkurugenzi mpya wa mamlaka hiyo ya maji (KASHWASA) Mhandisi Patrick Nzamba, alisema atachapa kazi kwa bidii na kuendeleza pale alipoishia Mstaafu Mhandisi Joshua Mgeyekwa, na kutoa huduma stahiki ya maji kwa kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama.

“Kazi hii ya kutoa huduma stahiki ya maji itafanikiwa endapo kama tutashirikiana pamoja na watumishi, bodi ya wakurugenzi, na wadau wa maji, hivyo naomba mnipe ushirikiano wa kutosha kama mlivyokuwa mkifanya kwa aliyenikabidhi kiti Mhandisi Mgeyekwa,”alisema Nzamba.

“Nitafanya kazi vizuri kwa kuhakikisha maeneo yote ambayo hayana huduma ya maji safi na salama kutoka Ziwa Victoria yanapata huduma hii, na yale ambayo tayari yana huduma tutaendelea kuboresha zaidi na kutoa huduma nzuri,”aliongeza.

Kwa upande wake Mstaafu Mhandisi Joshua Mgeyekwa, alisema anashukuru wafanya kazi wa Mamlaka hiyo kwa kumuunga mkono katika kipindi chake cha utumishi (KASHWASA) na kuwa mafanikio yote ambayo ameyapata yanatokana na umoja wao na kushirikiana katika kazi.

“Kipindi changu chote cha utumishi katika Sekta hii ya maji tangu mwaka (1990- 2022) ndani ya miaka 32, watu zaidi ya milioni 3 wamenufaika na huduma ya kupata majisafi na salama, “najivunia kwakweli” na mafaniko haya yanatokana na kuwa wamoja,”alisema Mhandisi Mgeyekwa.

“Nawaachia Nasaha watumishi wa KASHWASA. muendelee kufanya kazi kwa bidii na kuheshimu kanuni za kazi,”aliongeza.

Aidha, Mhandisi Joshua Mgeyekwa alianza kufanya kazi katika Wizara ya Maji mwaka (1990-1993), na mwaka (1994-2007) akaenda Mamlaka ya Maji Arusha, na mwaka (2007-2017) akahamia Mamlaka ya Maji Tanga, ambapo mwaka (2017) ndipo akahamia KASHWASA hadi kustaafu kwake 2022 na atakwenda kuishi Njombe.

Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi akizungumza kwenye hafla ya kuagwa Mstaafu Mhandishi Joshua Mgeyekwa ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji (KASHWASA).

Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi (KASHWASA) Mhandisi Bashir Mrindoko akizungumza kwenye hafla hiyo.

Mstaafu Mhandisi Joshua Mgeyekwa akizungumza kwenye hafla hiyo ya kuagwa kutumikia utumishi wa umma.

Mkurugenzi Mpya wa Mamlaka ya Maji (KASHWASA)Mhandisi Patrick Nzamba akizungumza kwenye hafla hiyo.

Mkurugenzi mpya wa Mamlaka ya maji (KASHWASA) Mhandisi Patrick Nzamba (kulia), akikata keki na Mhandisi Joshua Mgeyekwa ambaye alikuwa Mkurugenzi wa mamlaka hiyo na sasa amestaafu wakikata keki ili kufungua hafla hiyo ya kumuaga.

Muonekano wa keki.

Mkurugenzi mpya wa Mamlaka ya Maji (KASHWASA) Mhandisi Patrick Nzamba, (kulia) akimlisha keki Mstaafu Mhandisi Joshua Mgeyekwa ambaye amemuachia kiti cha (KASHWASA) kwenye hafla hiyo.

Mstaafu Mhandishi Joshua Mgeyekwa (kushoto)akimlisha keki Mhandisi Patrick Nzamba ambaye amemuachia kiti cha ukurugenzi katika Mamlaka ya Maji (KASHWASA).

Viongozi kutoka Taasisi za Serikali na Taasisi za kifedha, wakiwa kwenye hafla hiyo ya kuagwa Mhandisi Joshua Mgeyekwa ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji (KASHWASA) na sasa amestaafu.

Hafla ya kuagwa mstaafu Mhandisi Joshua Mgeyekwa ikiendelea.

Hafla ya kuagwa mstaafu Mhandisi Joshua Mgeyekwa ikiendelea.

Hafla ya kuagwa mstaafu Mhandisi Joshua Mgeyekwa ikiendelea.

Hafla ya kuagwa mstaafu Mhandisi Joshua Mgeyekwa ikiendelea.

Hafla ya kuagwa mstaafu Mhandisi Joshua Mgeyekwa ikiendelea.

Hafla ya kuagwa mstaafu Mhandisi Joshua Mgeyekwa ikiendelea.

Hafla ya kuagwa mstaafu Mhandisi Joshua Mgeyekwa ikiendelea.

Hafla ya kuagwa mstaafu Mhandisi Joshua Mgeyekwa ikiendelea.

Hafla ya kuagwa mstaafu Mhandisi Joshua Mgeyekwa ikiendelea.

Hafla ya kuagwa mstaafu Mhandisi Joshua Mgeyekwa ikiendelea.

Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi, (kulia) akimpatia zawadi Mstaafu Mhandisi Joshua Mgeyekwa kwenye hafla hiyo.

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi (KASHWASA) Mhandisi Bashir Mrindoko (kushoto) akimkabidhi zawadi ya Laptop ya kisasa, Mstaafu Mhandisi Joshua Mgeyekwa kwa niaba ya watumishi wa (KASHWASA).

Mkurugenzi Mpya wa (KASHWASA) Mhandisi Patrick Nzamba, (kushoto) akimkabidhi picha iliyochorwa Sura yake, Mstaafu Mhandisi Joshua Mgeyekwa, kwa niaba ya watumishi wa Mamlaka hiyo.

Mstaafu Mhandisi Joshua Mgeyekwa, akiwa ameshika picha iliyochorwa sura yake, zawadi ambayo amepewa na watumishi wa (KASHWASA) ambao alikuwa akiwaongoza kabla ya kustaafu.

Mstaafu Mhandisi Joshua Mgeyekwa, akiwa ameshika Tuzo ambayo amepewa na watumishi wa (KASHWASA) kutokana na kuwaongoza vyema.

Zawadi zikiendelea kutolewa.

Zawadi zikiendelea kutolewa.

Zawadi zikiendelea kutolewa.

Zawadi zikiendelea kutolewa.

Burudani ikiendelea kwenye hafla hiyo.

Burudani ikiendelea kwenye hafla hiyo.

Mstaafu Mhandisi Joshua Mgeyekwa, (kushoto) akipiga picha ya pamoja na Mhandisi Patrick Nzamba ambaye amemuachia kiti cha ukurugenzi Mamlaka ya Maji KASHWASA.
 
Na Marco Maduhu, SHINYANGA.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464