MBUNGE HANJE ATAKA KUJUA GHARAMA ZINAZOTUMIWA KWENYE MBIO ZA MWENGE WA UHURU


Mbunge wa Viti Maalumu, Nusrat Hanje ameibua sakata la mbio za mwenge akitaka kujua gharama zainazotumiwa na kama zitakuwa zinakaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).


Hata hivyo, Naibu Spika wa Bunge, Mussa Zungu amemjibu kuhusu umuhimu wa mwenge huo, akisema una maanufaa makubwa kwani unakagua miradi ya maendeleo na yenye ubora wa chini inakataliwa na kwamba, wakimbiza mwenge wanamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano.

Hanje ameibua hoja hiyo jana Jumatano April 6, 2022 wakati akichangia hotuba ya makadilio ya mapato na matumizi kwa Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zake ambapo ameomba mbio za mwenge zitazamwe upya.

Mbunge huyo amesema hana shida na umuhimu wa mbio za mwenge lakini shaka yake ni kiwango cha fedha kinachotumika kwa ajili ya ukimbizaji wa mwenge ambao gharama zake huwa haziwekwi hadharani katika matumizi yake ikiwemo kukaguliwa.

 SOMA HAPA ZAIDI CHANZO MWANANCHI.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464