MBOWE AGEUKA MBOGO RIPOTI YA CAG

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ameitaka Serikali kuwashughulikia watu wote waliolisababishia Taifa hasara ya mabilioni ya fedha kama ilivyobainishwa kwenye ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

 

Mbowe alieleza hayo juzi katika Kata ya Sinza, wilayani Ubungo akiwa kwenye kampeni ya ‘Join the Chain’ yenye lengo la kuhamasisha wananchi kukichangia chama hicho kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kujiimarisha na kujijenga.

Hayo yanajiri siku chache baada ya CAG, Charles Kichere kuwasilisha ripoti yake bungeni ikibainisha upotevu na ubadhirifu wa fedha jumla ya Sh5.8 trilioni kwenye mashirika na taasisi za umma, Serikali za mitaa na Serikali Kuu.

SOMA HAPA ZAIDI CHANZO MWANANCHI.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464