NDOA YA WATOTO WA UMRI WA MIAKA 12 NA 16 YATIBULIWA WAZAZI WATIWA MBARONI




Picha siyo ya tukio halisi.

NDOA ya watoto wawili iliyopangwa kufungwa kati ya mume mwenye umri wa miaka 12 na mke wa miaka 16, imetibuka katika hatua za mwisho katika kijiji cha Getarungu, Serengeti mkoani Mara.

Ndoa hiyo imetibuliwa na Jeshi la Polisi wilayani humo huku likiwanasa watu saba, wakiwamo watoto hao ambao ni wanafunzi wa Shule ya Msingi Kitarungu wilayani Serengeti mkoani Mara.

Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu juzi, Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Dk. Vincent Mashinji, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo siku tatu zilizopita.

Dk. Mashinji ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Serengeti, alisema ndoa hiyo ilitibuka dakika za mwisho kabla haijafungwa.

Alisema ndoa hiyo ilitarajiwa kufungwa kimila na iliingia doa bada ya vyombo vya dola kuvamia na kuwakamata watu waliohusika nayo.

taarifa zilizokuwa zimetolewa na jeshi la polisi na kuthibitishwa na Dk. Mashinji zilisema watu hao walikamatwa baada ya polisi kupata taarifa za kiintelijensia kwamba watuhumiwa wote, wakiwamo watoto waliotaka kufunga ndoa pamoja na wasimamizi wao, walikamatwa nyumbani kwa bwana harusi.

Watu wanaoshikiliwa katika tukio hilo ni pamoja na Nyang'ombe Magere (50), Ghati Masero (38) ambao ni wazazi wa mtoto wa kiume aliyekuwa anaoa. Wengine ni Kibaki Rioba (23), mkazi wa Sirari wilayani Tarime na watoto wenye umri wa miaka 12 na 16 waliokuwa wanaoana.

SOMA ZAIDI HAPA CHANZO NIPASHE.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464