SHIRIKA LA RAFIKI- SDO LAWAJENGEA UWEZO WANA-TAPO SHINYANGA JUU YA UJUZI WA MALEZI NA MAKUZI YA WATOTO

Mwezeshaji wa mafunzo ya malezi na makuzi ya watoto Sabrina Majikata kutoka Shirika la ICS mkoani Shinyanga akitoa elimu kwa wana -TAPO.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

SHIRIKA la Rafiki -SDO mkoani Shinyanga, limeendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo muungano wa mashirika yasiyo ya kiserikali (TAPO), yanayofanya afua za kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto wilayani Shinyanga, juu ya ujuzi malezi na makuzi ya watoto katika kutekelekeza maeneo makuu ya MTAKUWWA.

Mafunzo hayo ambayo yatachukua muda wa siku mbili, yameanza kufanyika leo, April 5, 2022 katika Hoteli ya Liga iliyopo Mjini Shinyanga, na kuhusisha wana-TAPO kutoka Mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali.

Mratibu wa mradi tuwalee kutoka Shirika hilo la Rafiki- SDO Maria Maduhu, amesema wameendesha mafunzo hayo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wao, ambao umelenga kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

“Shirika la Rafiki- SDO tunatekeleza mradi wa tuwalee kwa ufadhili wa mfuko wa Ruzuku wa wanawake Tanzania (WFT-Trust), ambao ni wa miezi mitano ulianza januari mwaka huu na utaisha mwezi mei kwa gharama ya Sh.milioni 29,”anasema Maduhu.

“Moja ya utekelezaji wa mradi huu ni kuwajengea uwezo wana-TAPO Juu ya masuala ya malezi na makuzi ya watoto katika kutekeleza Afua za MTAKUWWA, ili watakapokuwa kwenye utekelezaji wa miradi yao watoe elimu hii kwa usahihi,”ameongeza.

Kwa upande wake mwezeshaji wa mafunzo hayo Sabrina Majikata kutoka Shirika la Investing in Children and Strengthening Their Societies (ICS), amesema ili Taifa liwe imara lazima kuwe na familia bora ambayo haina matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto pamoja na kulinda ustawi wa mtoto na kumpatia malezi bora.

“Mafunzo ambayo nayatoa kwa wana-TAPO hawa, nimezingatia ajenda ya kitaifa ya malezi, ambayo inaitwa familia bora Taifa imara, na tukiwa na familia bora lazima Taifa litakuwa imara.”anasema Sabrina.

Aidha, Sabrina alitumia fursa hiyo pia kutoa wito kwa wazazi mkoani Shinyanga, kuzingatia malezi bora ya watoto wao ili wakue na afya njema, pamoja na kuwalinda dhidi ya magonjwa mbalimbali likiwamo janga la virusi vya ukimwi.

Katika hatua nyingine, amewataka pia wazazi kupanga uzazi wa mpango kwa kuzaa watoto na kuacha nafasi angalau miaka miwili, ili wapate nafasi ya kulea watoto wao vizuri na kuwapatia lishe na malezi bora, pamoja na wajawazito kupenda kujifungulia kwenye vituo vya afya sehemu ambayo ni salama na kupata elimu ya afya ya uzazi.

Na baadhi ya wana TAPO hao, walisema mafunzo hayo yamekuwa msaada mkubwa sana katika utekelezaji wa miradi yao ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto na kuifanya jamii iishi salama na familia bora.
Mwezeshaji wa mafunzo ya malezi na makuzi ya watoto Sabrina Majikata kutoka Shirika la ICS mkoani Shinyanga akitoa elimu kwa wana- TAPO.

Elimu ikiendelea kutolewa.
Mratibu wa mradi tuwalee kutoka Shirika la Rafiki- SDO Maria Maduhu, akielezea madhumuni ya mafunzo hayo kwa wana-TAPO na lengo la mradi wao.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo.

Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo.

Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo.

Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo.

Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo.

Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo.

Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo.

Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo.

Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo.

Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo.

Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo.

Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo.

Picha ya pamoja ikipigwa mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo kwa siku ya kwanza, ambayo yatahitimishwa kesho.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464