BAVICHA SHINYANGA WAFUNGUKA HALIMA MDEE NA WENZAKE 18 WAFUKUZWE BUNGENI

Mwenyekiti wa BAVICHA Jimbo la Shinyanga Mjini Samsoni Ngw'agi.

Wabunge 19 wa vitimaalum waliofukuzwa CHADEMA

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

BARAZA la vijana la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema (BAVICHA) Jimbo la Shinyanga Mjini, limemuomba Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Tulia Acksoni kuwafukuza Bungeni Halima Mdee pamoja na wezake 18, kwa madai kuwa siyo wabunge halali wa vitimaalum ambao wanatokana na chama hicho.

Mwenyekiti wa Baraza hilo Samsoni Ng’wagi amebainisha hayo leo Mei 12, 2022 wakati akizungumza na vyombo vya habari, kufuatia Baraza kuu la Chadema kusikiliza Rufaa ya akina Halima Mdee na wenzake 18, na kufikia hatua ya kuwafukuza ndani ya chama hicho mara baada ya wajumbe kupiga kura nyingi za kuwakataa.

Amesema hiyo ni mara ya pili wanafukuzwa ndani ya Chama hicho, na kuliomba Bunge litii miongozo ya katiba na maamuzi ya Chadema, kuwa Halima Mdee na wenzake 18 hawatakiwi kuendelea kuwepo Bungeni, sababu wameshafukuzwa na hawana chama cha kuwafanya kuwa ndani ya bunge.

“Halima Mdee na wenzake 18 kuendelea kuwepo ndani ya Bunge ni kuiibia fedha Serikali, na ni mafisadi kama mafisadi wengine tu, hivyo tunamuomba Spika wa Bunge Dk, Tulia Acksoni asimamie sheria na kuwatimua Bungeni, na fedha zote ambazo wamelipwa na bunge wazirudishe ili zikatekeleze miradi ya maendeleo,”amesema Ngw’agi.

Aidha, amekipongeza Chama chake kwa hatua hiyo ya kuwafukuza Halima Mdee na wenzake 18, na kuomba wachukuliwe pia hatua kali za kisheria kwa kugushi nyaraka za Chama hicho, ili liwefundisho kwa wengine pamoja na kuchunguza wasaliti wengine ambao wapo nyuma yao na kisha kuwafukuza na kukisafisha chama.

Baraza kuu la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jana walikaa kikao kusikiliza Rufaa ya akina Halma Mdee na wenzake 18 ya kupinga kufukuzwa ndani ya Chama hicho, ambapo wajumbe walipiga kura na kura 413 za wajumbe hao waliunga mkono wafukuzwe, huku kura Tano ndiyo zilipinga kutofukuzwa.

Upigaji wa kura ulivyokuwa kwa kila Kanda na Matokeo yake.

*Kanda ya Victoria Wajumbe 44*

-Wanaokubalia wavuliwe uwanachama 42

-Wasiokubali 1

-Wasiofungamana na Upande wowote 1

_*Jumla kura 44*_

*Kanda ya Nyasa Wajumbe 57*

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 57

-Wasiokubalina 0

-Wasifungamana na Upande wowote 0

_*Jumla ya Kura 57*_

*Kanda ya Unguja Wajumbe 22*

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 19

-Wasiokubali 1

-Wasifungamana na Upande wowote 1

_*Jumla ya Kura 22*_


*Kanda ya Pemba 15*

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 12

-Wasiokubali 1

-Wasifungamana na Upande wowote 2

_*Jumla ya Kura 15*_



*Kanda ya Kusini 32*

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 32

-Wasiokubali 0

-Wasifungamana na Upande wowote 0

_*Jumla ya Kura 32*_

*Kanda ya Pwani 47*

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 45

-Wasiokubali 0

-Wasifungamana na Upande wowote 2

_*Jumla ya Kura 47*_

*Kanda ya Kati 44*

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 44

-Wasiokubali 0

-Wasifungamana na Upande wowote 0

_*Jumla ya Kura 44*_

*Kanda ya Serengeti Wajumbe 41*

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 41

-Wasiokubalina 0

-Wasifungamana na Upande wowote 0

_*Jumla ya Kura 41*_

*Kanda ya Magharibi Wajumbe 37*

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 37

Wasiokubali 0

Wasifungamana na Upande wowote 0

_*Jumla ya Kura 37*_

*Kanda ya Kaskazini Wajumbe 61*

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 61

-Wasiokubali 0

-Wasifungamana na Upande wowote 0

*Jumla ya kura 61*

*Kamati Kuu*

Wanaokubali wavuliwe uanachama 23

Wasiokubali 0

Wasiofungamana 0

*Jumla ya kura 23*


*Wanaounga mkono wafukuzwe uanachama kura 413*

*Wasiounga mkono kufukuzwa kura 5*

*Wasiofungamana na upande wowote kura 5*

*Jumla ya kura zilizopigwa 423*
 
Halima Mdee na wenzake 18 waliingia ndani ya Bunge Kama Wabunge wa Vitimaalum kupitia CHADEMA, ambapo Chama hicho kilikataa kupeleka wabunge bungeni, kwa madai ya kutoridhishwa na matokeo ya uchaguzi Mkuu 2020.


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464