DC MBONEKO AKABIDHI VITI, MEZA NA STULI KITUO KIPYA CHA POLISI MWAKITOLYO

 Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Polisi wilaya ya Shinyanga John Kafumu (kushoto), Viti, Meza na Stuli za mapokezi kwa ajili ya matumizi ya Askari Polisi katika kituo kipya cha Polisi Mwakitolyo wilayani Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MKUU wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, amekabidhi viti, meza na stuli za mapokezi, kwa ajili ya matumizi ya Askari katika kituo kipya cha Polisi kilichopo Mwakitolyo wilayani Shinyanga.


Mboneko amekabidhi Samani hizo leo Mei 6, 2022 kwa Mkuu wa Polisi wilaya ya Shinyanga John Kafumu, ambazo zimetolewa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kahama na Shinyanga (KASHWASA).


Akizungumza wakati wa kukabidhi samani hizo, amewapongeza wadau hao (KASHWASA) kwa kutoa viti vinane, meza nane na stuli nne za mapokezi, kwa ajili ya matumizi ya Askari katika kituo hicho kipya cha Polisi Mwakitolyo, ambacho kitasaidia kuimalisha ulinzi na kudumisha amani.

“Ujenzi wa kituo kipya cha Polisi Mwakitolyo umeshakamilika na kuanza kutumika, na kitazinduliwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru, na nilitafuta wadau kwa ajili ya kutuchangia viti, meza na stuli za mapokezi kwa ajili ya matumizi ya Askari wetu, na leo na kabidhi rasmi kwa Jeshi la Polisi,”alisema Mboneko.

“Kituo hiki cha Polisi Mwakitolyo ni muhimu sana, sababu shughuli kubwa za wananchi wa eneo hilo ni wachimbaji wa madini ya dhahabu, na wakiuza dhahabu fedha zao zitakuwa salama, pamoja na amani kutawala sababu kutakuwa na ulinzi madhubuti,”aliongeza.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo ya Maji (KASHWASA) Nicholaus Oyier, alisema wameguswa kutoa thamani hizo kwa ajili ya matumizi ya askari katika kituo hicho cha Polisi Mwakitolyo, ambacho kitasaidia pia kulinda miundombinu yao ya maji isihujumiwe.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Polisi wilaya ya Shinyanga John Kafumu (kushoto), Viti, Meza na Stuli za mapokezi kwa ajili ya matumizi ya Askari Polisi katika kituo kipya cha Polisi Mwakitolyo wilayani.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (kushoto) akipokea Viti, Meza na Stuli za kaunta, kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa (KASHWASA) Nicholaus Oyier, kwa ajili ya kukabidhi kwa Jeshi la Polisi ili vikatumike katika kituo kipya cha Polisi Mwakitolyo.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (kushoto) akipokea Stuli za mapokezi, kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa (KASHWASA) Nicholaus Oyier kwa ajili ya kukabidhi kwa Jeshi la Polisi ili vikatumike katika kituo kipya cha Polisi Mwakitolyo.

Viti, Meza na Stuli ambavyo vimekabidhiwa kwa Jeshi la Polisi kwa ajili ya kwenda kutumika katika kituo kipya cha Polisi Mwakitolyo.

Mkuu wa Polisi wilaya ya Shinyanga John Kafumu, akiwa amekalia kiti na meza ambavyo vitakwenda kutumika katika kituo kipya cha Polisi Mwakitolyo wilayani Shinyanga, (kulia) ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (kushoto) Kaimu Mkurugenzi wa (KASHWASA) Nicholaus Oyier.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464