Picha : RAIS SAMIA ATEMBELEA BANDA LA MISA - TANZANIA MAADHIMISHO SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika Banda la Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania (MISA-TAN) kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ikiongozwa na kauli mbiu ‘Uandishi wa habari na changamoto za kidigiti' leo Jumanne Mei 3 ,2022 katika ukumbi wa Gran Melia Hotel Jijini Arusha. Kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania (MISA-TAN),Bi. Salome Kitomari akielezea akielezea malengo ya MISA - TANZANIA ambayo ni pamoja na kuhakikisha uhuru wa vyombo vya habari na upatikanaji wa taarifa unakuwepo,ukuaji wa vyombo vya habari imara vinavyowajibika na mazingira mazuri ya uandishi wa habari katika nchi wanachama kwa maendeleo na ustawi wa nchi.
Kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania (MISA-TAN),Bi. Salome Kitomari akimwelezea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan shughuli zinazofanywa na MISA - TANZANIA. Kitomari amesema MISA TANZANIA ni sehemu ya Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) yenye makao makuu yake nchini Zimbabwe ikiwa na matawi katika nchi tisa za SADC ambazo ni Malawi, Zambia, Zimbabwe, Botswana, Angola, Msumbiji, Lesotho,Afrika Kusini na Eswatn. Ilianzishwa mwaka 1991 kwa azimio la Windhoek, Namibia ambalo liliitambua siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani kama siku ya uhuru wa vyombo vya habari ikiwa ni miaka 31 sasa, na MISA ilipewa jukumu la kuhakikisha maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya habari duniani yanafanyika.
Kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania (MISA-TAN),Bi. Salome Kitomari akimwelezea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan shughuli zinazofanywa na MISA - TANZANIA. 

Soma pia :
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464