Afisa Miradi wa Shirika la TCRS Mwanamina Jumanne akiwa ameshika Taulo za kike na kutoa elimu ya matumizi yake kabla ya kuanza kugawia wanafunzi.
Na Mwandishi wetu, KISHAPU
SHIRIKA la TCRS linalotoa ufadhili wa misaada mbalimbali kwa watu wanaoishi katika mazingira magumu, limetoa msaada wa Taulo za kike kwa wanafunzi wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, kwa lengo la kuwanusuru kukosa vipindi vya masomo wanapokuwa katika siku zao za hedhi.
TCRS wametoa msaada huo leo Mei 30, 2022 kwa kutembelea shule mbalimbali za Sekondari wilayani Kishapu, na kisha kuwapatia wanafunzi elimu ya Afya ya uzazi na msaada huo wa Taulo la kike kwa kushirikiana na Shirika la FELMFinnish Evangelical Lutheran Mision lenye makao yake makuu nchini Finland.

Afisa Ustawi wa Jamii Wilayani Kishapu Mwajuma Abeid, akitoa elimu kwa wanafunzi namna ya matumizi sahihi ya Taulo hizo za kike.
Rehema Jumanne Mratibu wa huduma za Afya ya uzazi kwa wanawake na Mtoto Wilaya ya Kishapu.akizungumza kwenye utoaji wa elimu Afya ya uzazi na ugawaji wa Taulo za kike.
Mwalimu mlezi Shule ya Sekondari Mwakipoya wilayani Kishapu Monica Esmail akizungumzia changamoto za ukosefu wa Taulo kwa watoto wa kike shuleni hapo.
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mangu wilayani Kishapu Leah Nhalango akitoa shukrani kwa kupata msaada wa Taulo hizo za kike.
Wanafunzi wakiwa wameshika Taulo za kike ambazo wamepewa msaada na Shirika la TCRS.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464