WAHITIMU KIDATO CHA SITA DON BOSCO WAONYWA KUJICHANGANYA KWENYE MAKUNDI YASIYO NA MAADILI

Mgeni Rasmi Afisa Elimu watu wazima na Elimu nje ya Mfumo Rasmi Mkoa wa Shinyanga Mwl. Dedan William Rutazika akizungumza kwenye mahafali hayo.


Na Suzy Luhende, SHINYANGA

WANAFUNZI 37 waliohitumu kidato cha Sita katika shule ya Sekondari Don Bosco, wametakiwa kuacha kujichanganya kwenye makundi yasiyo na maadili, badala yake watumia elimu waliyopata kutatua Changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii, pamoja na kuelimisha masuala mbalimbali ya maendeleo.



Wito huo umetolewa jana na Afisa Elimu ya Watu wazima na Elimu ya nje ya Mfumo rasmi Dedan William Rutazika alipokuwa mgeni rasmi katika mahafari ya 21 ya kuwaaga wanafunzi wa kidato cha Sita iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Don Bosco iliyopo kata ya Didia halmashauri ya Shinyanga mkoani hapa.

Rutazika amesema wanamaliza kidato cha sita na kuelekea majumbani wanatakiwa wakawe mfano wa kuigwa wakaelimishe jamii juu ya masuala mbalimbali ya kimaendeleo,wasijiingize kwenye makundi mabaya, wasubiri matokeo yatakapotoka waweze kujiunga na vyuo vilivyopo ambavyo vipo vya kati na vya juu.

" Nawapongeza sana kwa kufikia hatua hii ya kuhitimu kidato cha sita kwenye risala mmesema mlianza mwaka 2020 mkiwa wanafunzi 42 lakini sasamnamaliza mkiwa 37 hongereni sana nawaomba mkawe kielelezo katika jamii, mkaelimishe masuala ya sensa ili watu wote waweze kushiriki zoezi la uandikishwaji" amesema Rutazika.

"Pia nimejionea mwenyewe hapa watoto wameonyesha vipaji mbalimbali naupongeza sana uongozi wa Shule hii kwa kutoa Elimu bora na vipaji mbalimbali, hivyo naomba muendelee kuwatoa vizuri nawaonyesha njia iliyobora"aliongeza Rutazika.

Aidha Rutazika amesema kuwa serikali ya awamu ya sita, inatambua mchango wa Shule binafsi kwani zinasaidia katika kupunguza uhaba wa Shule nchini na kuboresha Elimu nchini.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule hiyo Padri Felix Wagi amewataka Wahitimu kuwa na utulivu wa mwili na akili, baada ya kufanya mahafari yao ili waweze kufanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho.

Justin Msaiye katibu wa elimu jimbo la Kahama, Paroko wa parokia ya Kagongwa Kahama aliyeongoza misa ya kuwaaga wanafunzi wa kidato cha sita aliwataka wakaendelee kuwa na maadili mema huko waendako kama waliuofundishwa shuleni hapo.

Baadhi ya wanafunzi waliohitimu kidato cha sita Diana Nzwala na Zakalia Lukas walisema kwa sababu wamefundishwa maadili mema katika shule hiyo, hivyo wanaamini watafanya vizuri pale watakapoenda majumbani na wataendelea kumuomba Mungu ili waweze kufaulu vizuri na kisonga mbele

Mahafali hayo ya 21 ambayo yalikuwa na jumla ya Wahitimu 37, yamefanyika katika viwanja vya Shule hiyo na kutanguliwa na Ibada misa takatifu iliyoongozwa na Padiri Justine Msaiye, paroko wa parokia ya Kagongwa Kahama.

Mgeni Rasmi Afisa Elimu watu wazima na Elimu nje ya Mfumo Rasmi Mkoa wa Shinyanga Mwl. Dedan William Rutazika akizungumza kwenye mahafali hayo.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Don Bosco Didia Shinyanga Fr. Felix Wagi akizungumza katika mahafali hayo.

Mgeni Rasmi katika picha ya pamoja na Wahitimu pamoja na watumishi wa Shule ya Sekondari Don Bosco Didia Shinyanga.

Wahitimu 37 wa kidato cha Sita shule ya Sekondari Don Bosco Didia wakitoa burudani.

Mahafali yakiendelea.









Na Suzy Luhende, SHINYANGA.


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464