Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (kulia) akimpatia Chanjo ya Polio Mtoto wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo la Chanjo mkoani Shinyanga.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, amezindua zoezi la utoaji Chanjo ya Polio kwa watoto waliochini ya umri wa miaka mitano, ili kuwakinga na ugonjwa wa kupooza utokanao na virusi vya Polio, huku akiwatoa hofu wazazi kuwa Chanjo hiyo ni salama.
Mjema akizungumza wakati wa uzinduzi wa Chanjo hiyo, amewasihi wazazi mkoani humo, wapeleke watoto wao kwa wingi wakapate Chanjo, ambayo itawakinga dhidi ya ugonjwa wa kupooza utokanao na virusi vya Polio.
“Niwatoe hofu wazazi wa Mkoa huu wa Shinyanga, Chanjo hii ya Polio ni salama kabisa na haina madhara yoyote, hivyo wapelekeni watoto wenu wakapate Chanjo ambayo hutolewa kwa njia ya matone na kubaki kuwa salama, sababu ugonjwa huu upo tu hapa nchi ya jirani Malawi,”amesema Mjema.
“Ugonjwa huu wa kupooza una ambukizwa kwa kirusi cha Polio kwa kula chakula, kunywa maji machafu au kinyesi, na watoto ndiyo wapo katika hatari kubwa kutokana na kula hovyo hasa wanapokuwa wakicheza, na ndiyo maana wanapatiwa Chanjo,”aliongeza.
Kwa upande wake Carle Lyimo kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), naye amekazia Chanjo hiyo ni salama, na kuelezea kuwa imekuja kwa ajili ya kumkomboa mtoto wa Mtanzania kutokana na ugonjwa huo kuathiri watoto wa nchi jirani ya Malawi.
“Ugonjwa huu upo nchi jirani ya Malawi, na kuna muingiliano mkubwa wa kibiashara, na ndiyo maana tunasisitiza sana watoto wetu wapatiwe Chanjo ya Polio,”amesema Lyimo.
Aidha, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Yudas Ndugile alisema Chanjo hiyo ya Polio mkoani Shinyanga inatarajia kufikia watoto 450,000 walio na umri chini ya miaka mitano, na itatolewa kwenye vituo vya afya, maeneo yenye mikusanyiko ya watu, pamoja na nyumba kwa nyumba ili kufikia malengo kusudiwa.
Nao baadhi ya wazazi mkoani Shinyanga ambao watoto wao wamepatiwa Chanjo hiyo ya Polio kwenye uzinduzi huo, wametoa wito kwa wazazi wenzao kuwa waitikie zoezi hilo na kupeleka watoto wao kupata Chanjo, na kuwalinda dhidi ya ugonjwa huo wa kupooza.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (kulia) akimpatia Chanjo ya Polio Mtoto wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo la Chanjo mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (kulia) akimpatia Chanjo ya Polio Mtoto wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo la Chanjo mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (kulia) akimpatia Chanjo ya Polio Mtoto wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo la Chanjo mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (kulia) akimpatia Chanjo ya Polio Mtoto wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo la Chanjo mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (kulia) akimpatia Chanjo ya Polio Mtoto wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo la Chanjo mkoani Shinyanga.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, (kulia) akimpatia Chanjo ya Polio Mtoto wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo la Chanjo ya Polio mkoani Shinyanga.
Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Ester Makune, (kulia) akimpatia Chanjo ya Polio Mtoto wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo la Chanjo ya Polio mkoani Shinyanga.
Diwani wa Vitimaalum Manispaa ya Shinyanga Shela Mshandete (kulia) akimpatia Chanjo ya Polio Mtoto wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo la Chanjo ya Polio mkoani Shinyanga.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA.