Fred Paulo akiangalia samani za ndani ambazo zimeteketea wakati nyumba yao ikiungua moto
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
Watu nane wamenusirika kifo wakati nyumba ambayo wanaishi mtaa wa Mwinamila Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga ikiungua moto na kuteketeza kila kitu ndani.
Tukio hilo la Moto limetokea leo Mei 10, 2022 majira ya saa 11 jioni katika Mtaa wa Mwinamila Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga
Anasema moto huo ulianza kushika kwenye sofa, ndipo ikabidi akimbie kwenda kuzima umeme (Main Switch), na kuanza kuomba msaada kwa wasamaria wema kusaidia kuuzima moto huo, na kufanikiwa kuuzima huku ukiwa tayari umeshateketeza kila kitu ndani, lakini nyumba yao ikisalimika kuteketea.
“kwenye hii nyumba tunaishi jumla ya watu nane wakiwamo na wapangaji, na huu moto ulianza kuwaka kwenye chumba changu, na shukuru Mungu nyumba haijateketea yote bali tumepotea samani zote za ndani,”anasema Paul.
Naye shuhuda wa tukio hilo la Moto Osca Kunze, anasema alikuwa amekaa jirani na nyumba hiyo akimsubili mtu, lakini akasikia kelele nyumba hiyo inaungua moto, ndipo alipofika eneo la tukio na kuanza kusaidia kuuzima, huku watu wengine wakiendelea kwenda na kufanikiwa kuuzima.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa huo wa Mwinamila eneo ambalo nyumba imeungua moto Lukia Athumani, amewapongeza wananchi kwa kujitokeza kwa wingi na kuokoa nyumba hiyo isiteketee kwa moto, huku akilitupia lawama Jeshi la Zimamoto na uokoaji kwa kuchelewa kufika eneo la tukio, na moto huo kuzimwa na wananchi.
Alisema amesikitishwa na Jeshi la Zimamoto na uokoaji kwa kutopokea simu kwa wakati, na baada ya kupata taarifa hawakwenda kwa haraka na kuchelewa kufika eneo la tukio, na walipofika walikuwa wamepanda kwenye bodaboda bila ya kuwa na gari, na kusababisha wananchi kutaka kuwashushia kichapo lakini alizuia tukio hilo.
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji wilaya ya Shinyanga Stanley Luhwago, alikiri Jeshi hilo kukabiliwa na upungufu wa magari, na kubainisha kuwa wana gari moja la kuzimiamoto ambalo nalo kwa sasa ni bovu.
Alitolea pia ufafanuzi sakata la Askari wa Jeshi hilo kutaka kupigwa na wananchi wakati alipofika eneo la tukio bila kuwa na gari la kuzimia moto, alisema kuwa Askari huyo alikuwa na wenzake wakitoa mafunzo kwa wananchi namna ya kukabiliana na majanga ya moto karibu na eneo la nyumba hiyo iliyoungua moto, na walipopata taarifa ilibidi afike hapo haraka ilikutoa msaada wa awali.
Alisema katika matukio ya moto hua kuna vitu vingi vya kuwahi kutoa msaada, ikiwamo namna ya kuokoa vitu au watu wasidhurike na moto, na ndiyo maana Askari huyo aliwahi ili akatoe msaada wakati askari wengine wakifanya mawasiliano ya kupata gari la kuzimiamoto kutoka Jeshi la wananchi kambi ya Kizumbi.
Fred Paul akielezea namna moto ulivyoanza kuwaka kwenye nyumba yao.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwinamila Lukia Athumani akielezea tukio hilo la Moto.
Osca Kunze akielezea namna wananchi walivyofanikiwa kuzima moto.
Wananchi wakitaka kumshushia kichapo Askari wa Jeshi la Zimamoto mara baada ya kufikia eneo la tukio akiwa na Bodaboda bila ya kuwa na Gari la kuzimia moto.
Wananchi wakitaka kumshushia kichapo Askari wa Jeshi la Zimamoto mara baada ya kufikia eneo la tukio akiwa na Bodaboda bila ya kuwa na Gari la kuzimia moto.
Fred Paulo akiangalia samani za ndani ambazo zimeteketea wakati nyumba yao ikiungua moto.
Wananchi wakiwa eneo la tukio.
Wananchi wakiendelea kuuzima Moto.
Wananchi wakiendelea kuuzima Moto.
vitu vikiwa vimeteketea na moto.
vitu vikiwa vimeteketea na moto.
vitu vikiwa vimeteketea na moto.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464