Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa kwa Mwaka 2022 Sahil Geraruma amegoma kukabidhi Pikipiki kwa baadhi ya vikundi vya Madereva wa bodaboda ambao wamenufaika na mkopo wa asilimia 10 kutoka Halmashauri baada ya kushindwa kutafsiri Sheria za usalama Barabarani.
Mwenge wa Uhuru ukiwa Wilayani Babati Mkoani Manyara kwaajili ya kukagua miradi mbalimbali.
Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge wa uhuru Gereruma amesema lengo la
Serikali ni kuhakikisha asilimia 10 ya mpango wa kila Halmashauri
unawafikia walengwa ambao ni Vijana, wanawake pamoja na watu wenye elemavu, lakini hawezi kuruhusu vijana kuingia barabarani wakiwa
hawafahamu sheria za usalama barabarani.
SOMA ZAIDI HAPA CHANZO millardAyo.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464