MEYA ALIYEKATALIWA NA MADIWANI ACHUKUWA TENA FOMU KUWANIA NAFASI HIYO

Juma Raibu akizungumza baada ya kuchukua fomu yakuwania nafasi ya Meya Manispaa ya Moshi

Meya wa zamani wa Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Juma Raibu aliyevuliwa wadhifa huo baada ya kupigiwa kura za siri na madiwani za kukataliwa amejitokeza tena kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania nafasi hiyo. 

Juma Raibu aling'olewa katika wadhifa huo Aprili 11 mwaka huu, baada ya madiwani kupiga kura za siri na kati ya kura 28 zilizopigwa, 18 zilikataa asiendelee na wadhifa huo huku 10 zikimtetea abaki katika nafasi hiyo aliyodumu nayo tangu ulipokamilika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

SOMA: Madiwani Moshi wamng'oa Meya madarakani, apanda bodaboda

Tuhuma zilizomng'oa Raibu ni madai ya kuhudhuria sherehe ya kijana mmoja anayedaiwa kushiriki mapenzi ya jinsia moja, kutumia vibaya ofisi yake, kujihusisha na vitendo vya rushwa, kuruhusu ujenzi holela na kutumia fedha nje ya utaratibu.

   soma zaidi hapa; Chanzo Mwananchi.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464