Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akizungumza kwenye Mahafali chuo cha VETA Shinyanga.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
MEYA wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, amekipongeza Chuo cha Elimu na Mafunzo ya ufundi Stadi VETA mkoani Shinyanga, kwa kazi nzuri ambayo wanaifanya ya kufundisha ujuzi vijana na kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira na kujiajiri wenyewe.
Amebainisha hayo leo June 3, 2022 katika Mahafali ya 38 wanafunzi wa chuo hicho cha VETA hatua ya Tatu, ambayo yamehudhuliwa na wazazi, maofisa elimu na viongozi mbalimbali.
Meya Masumbuko akizungumza kwenye Mahafali hayo, amesema anakipongeza chuo hicho cha VETA kwa kazi kubwa ambayo wanaifanya ya kuwapatia ujuzi vijana, na hata kujiajiri wenyewe na kupunguza tatizo la ajira, pamoja na kuunga mkono juhudi za Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassani ya ukuzaji Sekta ya viwanda.
“VETA Shinyanga mmekuwa mkifanya kazi kubwa sana ya kuzalisha wataalamu wenye ujuzi mbalimbali hapa Nchini, ambao wataendeleza Taifa hili katika Nyanja mbalimbali za kiujuzi na ukuzaji wa Sekta ya viwanda kwa kujiajiri wenyewe,”amesema Masumbuko.
“Sisi kama Serikali tutaendelea kuwa unga mkono vijana ambao wanahitimu hapa VETA kwa kuwapatia mikopo ya Halmashauri asilimia 10 ambayo kwa vijana hutolewa asilimia 4 ili wapate mitaji na kujiajiri wenyewe au kuwapatia vitendea kazi na kuendesha maisha yao na kuinuka kiuchumi na Taifa kwa ujumla,”ameongeza.
Aidha, akizungumzia changamoto ya mfumo wa Majitaka chuoni hapo amesema Manispaa ya Shinyanga ina gari la kusomba Majitaka, ambapo wataona namna ya chuo hicho kulitumia ili kupunguza gharama kubwa ambazo hukabiliana nazo kutokana na kukodisha gari la Majitaka.
Katika hatua nyingine Meya huyo, amewataka wahitimu kuwa huko watakapo kwenda uraiani wakadumishe nidhamu pamoja na kufanya kazi kwa bidii, ili kurinda heshima ya chuo hicho na siyo kwenda kufanya mambo ambayo hayastahili.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo hicho cha VETA Rashidi Ntahigiye ambaye ni Mratibu wa Mafunzo chuoni hapo, awali akisoma Taarifa ya chuo ametaja changamoto ambazo zinawakabili chuno hapo kuwa ni ukosefu wa mfumo wa Majitaka, upungufu wa mabweni kwa ajili ya kihifadhi wanafunzi na kusababisha baadhi yao kwenda kupanga magheto uraiani na wengine kushinda kumaliza mafunzo.
Ametaja changamoto zingine kuwa ni ukosefu wa kituo cha Afya, kutokuwepo na usafiri wa umma wa kusafirisha wanafunzi hadi chuoni, ambapo kipindi cha msimu wa mvua husababisha kuchelewa na hata kuacha kwenda chuo kabisa.
Naye Mwanafunzi wa Chuo hicho cha VETA Monica Ngowi akisoma Risala kwaniaba ya wahitimu wenzake, wameiomba Serikali kuangali namna ya kulegeza masharti ya upataji mikopo ya vijana kupitia Halmashauri asilimia 10, ili wapate mitaji na kujiajiri wenyewe na kuendesha maisha yao sababu ujuzi wanao.
Naye Kaimu Mratibu wa mafunzo chuoni hapo Tajiri Mollel, amesema wahitimu hao walianza mafunzo wakiwa 89 lakini wamehitimu 86 wasichana wakiwa 42 na wavulana 44 huku wanafunzi watatu wakishindwa kuhitimu kutokana na sababu mbalimbali.

Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akizungumza kwenye Mahafali Chuo cha VETA Shinyanga.
Kaimu Mkuu wa chuo hicho cha VETA Rashidi Ntahigiye ambaye ni Mratibu wa Mafunzo chuoni hapo, akisoma Taarifa ya chuo kwenye Mahafali hayo.
Kaimu Mratibu wa mafunzo Chuo cha VETA Shinyanga Tajiri Mollel, akisoma Taarifa ya mafunzo kwenye Mahafali hayo.
Mwanafunzi wa Chuo cha VETA Monica Ngowi akisoma Risala kwa niaba ya wahitimu wenzake kwenye Mahafali hayo.
Viongozi meza kuu wakiwa kwenye mahafali hayo.
Wahitimu wakiwa kwenye Mahafali.
Wahitimu wakiwa kwenye Mahafali.
Wahitimu wakiwa kwenye Mahafali.
Awali Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, akitembelea kuona Fani ya ubunifu na ushonaji wa mavazi chuoni hapo.
Awali Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, akitembelea kuona Fani ufundi umeme chuoni hapo.
Awali Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, akitembelea kuona Fani ya ukataji na ung'arishaji madini ya VITO chuoni hapo.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akitunuku vyeti wahitimu.
Zoezi la kutunuku vyeti wahitimu likiendelea.

Wahitimu wakitoa burudani ya ubunifu wa mavazi kwenye mahafali hayo.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464