Waziri wa fedha na Mipango Dk Mwigulu Nchemba
Waziri wa
Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema Serikali inakusudia kutoa namba ya
utambulisho wa mlipakodi (TIN) kwa kila Mtanzania mwenye umri wa kuanzia miaka
18 kuanza kulipa kodi.
Dk Mwigulu amebainisha hayo bungeni jijini Dodoma, wakati akiwasilisha mapendekezo ya Serikali
kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2022/23.
Waziri huyo amesema ili kufikia azma hiyo
wataanza kutoa namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN) kwa kila mtanzania
kuanzia umri wa kuanzia miaka 18 kwa utaratibu wa usajili wa namba ya
utambulisho wa Taifa (NIDA) unaomtaka kila mwananchi mwenye umri huo wa au
zaidi kujisajili.
SOMA ZAIDI HAPA-Chanzo Mwananchi