RC MJEMA AMPONGEZA RAIS SAMIA KUTOA FEDHA ZA RUZUKU KUPUNGUZA BEI YA MAFUTA, AWATAKA WANANCHI KUPUUZA MANENO YA UPOTOSHAJI


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza na wananchi wa Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga kwenye mkutano wa hadhara.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassani, kwa kutoa fedha za Ruzuku ya Mafuta Sh.bilioni 100 na kusababisha bei ya mafuta kushuka, na kupunguza makali ya maisha kwa wananchi.

Mjema ametoa pongezi hizo leo June 9, 2022, wakati akizungumza na Wananchi wa Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga kwenye mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi, mkutano uliohudhuliwa pia na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali.

Amesema kume kuwepo na upotoshaji mwingi juu ya kupanda kwa bei ya bidhaa mbalimbali hapa nchini yakiwamo mafuta, kuwa Serikali ndiyo imepandisha bei hizo, na kuwataka wananchi kupuuza maneno hayo kuwa siyo kweli, bali kupanda wa bidhaa hizo inatokana na Vita ya Ukraine na Urusi pamoja na ugonjwa wa UVIKO-19.

Mjema amesema kutokana na kupanda bei ya bidhaa hizo Rais Samia ametafuta pesa na kuamua kutoa Sh.bilioni 100 kwenye Ruzuku ya Mafuta, na kupelekea mafuta kushuka bei na kupunguza gharama za maisha kwa wananchi.

“Wananchi wa Shinyanga niwaambieni Rais wetu anatupenda sana, ameona wananchi wake wanateseka kwa kupanda kwa bei ya bidhaa mbalimbali yakiwamo mafuta, ikabidi akae na watalaamu wake na kisha kutafuta pesa na ameweka Sh.bilioni 100 kwenye Ruzuku ya mafuta na sasa yameshuka bei, nani kama Rais Samia mpigieni makofi Rais wetu,”amesema Mjema.

“Huyu ndiye Rais wa kimkakati mwanamke shupavu, ndani ya mwaka wake mmoja Madarakani amefanya mambo makubwa, na Tanzania kwa sasa tuna maendeleo makubwa kila Sekta mama amemwaga hela tunampongeza sana Rais wetu,”ameongeza Mjema.

Aidha, amesema katika Mkoa huo wa Shinyanga Rais Samia ametoa fedha nyingi, na kutekelezwa katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwamo ya Elimu, Afya, Umeme, Maji, Kilimo, Miundombinu ya Barabara, pamoja na kutoa fedha Sh. bilioni 15 kujenga uwanja wa Ndege Ibadakuli, na sasa Sh. bilioni 3.5 zimeshaanza kufanya kazi na Mkandarasi yuko kazini.

Katika hatua nyingine Mjema, amewahamasisha wananchi wa Mkoa huo wa Shinyanga siku ya zoezi la kuhesabiwa Sensa ya watu na makazi litakalofanyika Agost 23 mwaka huu, wajitokeze kwa wingi kuhesabiwa, ili Serikali ipate idadi ya watu wake kamili kwa kila eneo, na kuirahishia katika upangaji wa mipango yake ya maendeleo kwa wananchi.

Mkuu huyo wa Mkoa pia amewahamasisha wananchi waendelee kujitokeza kwa wingi kupata Chanjo ya UVIKO-19 ili siku wakipata maambukizi ya Corona wasipate madhara makubwa.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye mkutano huo wa hadhara, amesema Serikali itaendelea kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza na wananchi wa Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga kwenye mkutano wa hadhara.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza na wananchi wa Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga kwenye mkutano wa hadhara.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza na wananchi wa Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga kwenye mkutano wa hadhara.

Meya wa Manispaa ya Shinyanga Ekias Masumbuko, akizungumza na wananchi wa Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga kwenye mkutano wa hadhara.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura, akizungumza na wananchi wa Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga kwenye mkutano wa hadhara.

Diwani wa Ngokolo Victor Mkwizu, akiwasilisha changamoto ambazo zinawakabili wananchi wa Kata wa Kata hiyo kwenye mkutano wa hadhara.

Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye mkutano wa hadhara Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga.

Wananchi wa Ngokolo wakiwa kwenye mkutano wa hadhara.

Wananchi wa Ngokolo wakiwa kwenye mkutano wa hadhara.

Wananchi wa Ngokolo wakiwa kwenye mkutano wa hadhara.

Wananchi wa Ngokolo wakiwa kwenye mkutano wa hadhara.

Wananchi wa Ngokolo wakiwa kwenye mkutano wa hadhara.

Wananchi wa Ngokolo wakipata Chanjo ya UVIKO-19 mara baada ya kumalizka mkutano huo wa hadhara wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema.

Wananchi wakiendelea kupata Chanjo ya UVIKO-19.

Wananchi wakiendelea kupata Chanjo ya UVIKO-19.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464