Waziri wa Fedha
na Mipango Dk Mwigulu Nchemba amependekeza kufutwa ada ya kidato cha tano na
cha sita hatua ambayo inalenga kuwapunguzia gharama Wazazi na kuwawezesha
wanafunzi wanaotoka katika familia duni kusoma.
Akiwasilisha
bungeni jijini Dodoma leo Juni 14/2022 makadirio ya mapato na matumizi ya
bajeti ya Serikali ya mwaka 2022/2023.Waziri wa fedha na Mipango Dk. Mwigulu
amesema kwa sasa wanafunzi wa kidato cha tano ni takribani 90,825 na kidato cha
sita ni 56,880 na mahitaji ya fedha ni Sh billion 10 3.
Amesema ili
kuwapunguzia gharama wazazi na walezi ada kuanzia wanafunzi wa kidato cha tano
na sita inafutwa,hivyo kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha sita elimu bila
malipo.