
Wauguzi wa nchi hiyo wanalipwa dola 18,000 za Zimbabwe kwa mwezi lakini hivi sasa kiwango hicho ni sawa na dola 55 pekee za Marekani.
Mishahara ya walimu ndiyo yenye nafuu kidogo na inafikia dola za Marekani 75 pekee .
"Ukweli ni kwamba wafanyakazi wanalipwa ujira mdogo. Wafanyakazi wanahangaika kutimiza mahitaji yao" amesema Tapiwanashe Kusotera, kiongozi wa chama cha wafanyakazi wa sekta ya afya nchini Zimbabwe.
Hapo Jumatatu wafanyakazi wa sekta hiyo waliandamana mbele ya ofisi za Bodi ya Huduma za Afya zilizopo kwenye moja ya hospitali kubwa kabisa nchini humo, wakiwa wamebeba mabango na kuimba nyimbo za malalamiko