ALIYEKUWA BOSI TPA ASOMEWA MASHTAKA AKIWA KITANDANI MUHIMBILI

 

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Madeni Kipande (66) amesomewa mashtaka ya kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh4.2 bilioni akiwa amelazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI), Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Amesomewa mashtaka akiwa kitandani leo Jumatatu Julai 4, 2022 baada ya kufanyiwa upasuaji wa mgongo katika hospitali hiyo.

Kesi dhidi yake inasikilizwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu Dar es Salaam, Ramadhani Rugemarila.

 SOMA HAPA ZAIDICHANZO MWANANCHI.


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464