WAJUMBE BODI YA MAJI ARUSHA ‘AUWSA’ WATEMBELEA MRADI WA KUTIBU NA KUCHAKATA TOPE KINYESI, WAIPONGEZA SHUWASA KUBUNI UZALISHAJI WA MBOLEA

Wajumbe wa Bodi ya Maji Arusha (AUWSA) wakipiga picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Maji Shinyanga (SHUWASA) wakiwamo na baadhi ya watumishi wa Mamlaka  zote mbili za Maji katika Mtambo wa kutibu na kuchakata tope kinyesi (Majitaka) mara baada ya kufanya ziara kwenye mtambo huo.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

WAJUMBE wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWSA),wametembelea mtambo wa kutibu na kuchakata Tope kinyesi (Majitaka) uliopo Nhelegani Kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga, ambao unasimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA).

Wajumbe hao wa Bodi ya Maji Arusha (AUWSA) wamefanya ziara hiyo leo Julai 12, 2022, wakiwa wameambatana na Menejimenti ya Mamlaka hiyo ya Maji Arusha, kwa lengo na kujifunza na kubadilishana mawazo juu ya utendaji kazi na Mamlaka ya Maji Shinyanga (SHUWASA).

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi kutoka Mamlaka hiyo ya Maji Arusha (AUWSA) Jackline Mkindi, amesema wamefanya ziara katika Mamlaka ya Maji Shinyanga (SHUWASA), ili kujifunza jinsi gani wanavyofanya kazi, pamoja na kutibu tope kinyesi (Majitaka) hadi kuwa bidhaa.

Amesema katika ziara hiyo wamejifunza vitu vingi vizuri kutoka (SHUWASA), ambapo wao kama Bodi ya Maji Arusha (AUWSA) watakwenda kuvifanyia kazi na kuongeza ufanisi wa utendaji kazi kwenye Mamlaka hiyo ya Maji Arusha.

“Tunaipongeza Mamlaka hii ya Maji Shinyanga (SHUWASA) kwa ubunifu wao mkubwa, kutoka kutiyatibu Majitaka na kugeuza kuwa Mbolea, huu ni ubunifu wa hali ya juu sana ambao sisi tumejifunza,”amesema Mkindi.

“Kilimo ni njia sahihi ya kukuza uchumi, na hapa nchini kumekuwapo na tatizo la uhaba wa mbolea, hasa kutokana na Vita ya Urusi na Ukraine, hivyo mradi huu wa Mbolea hapa SHUWASA ni fursa kubwa katika sekta ya kilimo,”ameongeza.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola, amesema katika ziara hiyo imekuwa na mafanikio pia kwao, ambapo wamebadilishana mawazo na kupeana ushauri wa kiutendaji kazi.

Amesema katika Mtambo huo wa kutibu na kuchakata tope kinyesi (Majitaka) waliamua kubuni mbinu ya kugeuza tope hilo na kuwa Mbolea kwa kushirikiana na Shirika la maendeleo la Uholanzi (SNV), Mbolea ambayo itatumika kuzalishia mazao mashambani.

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi kutoka Mamlaka ya Maji Arusha (AUWSA) Jackline Mkindi, akizungumza mara baada ya kuhitimisha ziara yao katika Mtambo wa kutibu na kuchakata tope kinyesi (Majitaka) uliopo Nhelegani Kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola akizungumza kwenye ziara hiyo ya Wajumbe wa Bodi ya Maji Arusha (AUWSA) katika Mtambo wa kutibu na kuchakata tope kinyesi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola akiendelea kuzungumza kwenye ziara hiyo ya Wajumbe wa Bodi ya Maji Arusha (AUWSA) katika Mtambo wa kutibu na kuchakata tope kinyesi.

Ziara ya Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Arusha (AUWSA) ikiendelea katika Mtambo wa kutibu na kuchakata tope kinyesi (Majitaka) uliopo Nhelegani-Kizumbi Manispaa ya Shinyanga.

Muonekano wa Mtambo wa kutibu na kuchakata tope kinyesi (Majitaka).

Gari likimwaga Majitaka katika Mtambo huo wa kutibu tope kinyesi.

Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWSA)wakiangalia Mbolea ambayo inatokana na tope kinyesi (Majitaka) ambayo itatumika kuzalishia mazao mbalimbali mashambani.

Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWSA) wakiwa ziara katika Mtambo wa kutibu na kuchakata tope kinyesi (Majitaka) Nhelegani-Kizumbi Manispaa ya Shinyanga.

Wajumbe wa Bodi ya Maji Arusha (AUWSA) wakipiga Picha ya Pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Maji Shinyanga (SHUWASA) wakiwamo na baadhi ya watumishi wa Mamlaka zote mbili za Maji katika Mtambo wa kutibu na kuchakata tope kinyesi (Majitaka) mara baada ya kufanya ziara kwenye mtambo huo.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464