Mahakama Kuu ya Tanzania imekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kufika Mahakamani kesho katika kesi ya Halima Mdee na wenzake 18 wanaopinga kuvuliwa uanachama wa chama hicho itakayotajwa mbele ya Jaji Cyprian Mkeha.
Mdee, ambaye alikuwa mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) na wenzake walifungua shauri hilo Julai 21 mwaka huu, ikiwa ni siku 13 baada ya kupata ridhaa ya mahakama hiyo.
Katika shauri hilo, wabunge hao wanapinga uamuzi wa Baraza Kuu la Chadema wa Mei 11, 2022 kuwavua uanachama, kwa utaratibu wa mapitio ya mahakama.
Juzi mahakama hiyo ilitoa hati ya wito ikiwataka wadaiwa katika shauri hilo kufika mahakamani kesho wakati shauri hilo litakapotajwa kwa ajili ya maelekezo muhimu, ikiwa ni hatua ya maandalizi ya usikilizwaji wake.
SOMA ZAIDI HAPA CHANZO MWANANCHI.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464