MADAKTARI BINGWA KUTOKA KOREA WAPIGA KAMBI MWANZA

 
Madaktari bingwa watatu wa magonjwa mbalimbali kutoka nchini Korea wakishirikiana na madaktari 9  kutoka Mkoa wa Mwanza wamepiga kambi kutoa huduma za afya bure kwa  wananchi waonakaa visiwa vilivyoko wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza.
 Makamu wa rais wa shirika hilo lisilokuwa la kiserikali kutoka nchini Korea la Christian Life World Mission Frontiers, Mathew Lubongeja amewasihi wananchi wote kujitokeza kupata huduma hiyo.

Pa ameishukuruku serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza kwa kuwapa ushirikiano tangu wamefika nchini na wakiendelea kutoa huduma kwa wananchi wanaoishi katika visiwa vya Ziwa Victoria.

Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Buchosa, Dk. Deus Dakama  amesema huduma hizo zimeanza  kutolewa Julai 5,2022 Kisiwani Kome kambi ya uvuvi ya Kome Mchangani inayotolewa bure na madaktari hao wakishirikiana na  madaktari wa Tanzania.
madaktari hao wakishirikiana na  madaktari Wa kitanzania.

Amesema wananchi wa maeneo hayo watapata huduma bure za vipimo na dawa kwa yoyote atayekutwa na ugonjwa.

Dk. Dakama amesema kwenye kambi ya uvuvi ya Kome Mchangani walipima zaidi ya 300 na ugonjwa mkubwa uliobainika kuwakabili wakazi wa maeneo hayo ni shinikizo la damu  na  kichocho  kutokana na wakazi hao kutumia maji yasiyo safi na salama.

" Jana tulianza mchangani leo tuko Ntama tunatoa huduma bure za afya kwa wananchi hivyo wananchi wanatakiwa kutojitokeza kwa wingi kupata huduma hiyo ",amesema Dk. Dakama.

Juma Hasani mmoja wa wakazi wa Kome Mchangani amesema wameridhishwa na matibabu yanayotolewa na madaktari kutoka Korea wakishirikiana na madaktari kutoka Tanzania.

Huduma hiyo inatolewa na madaktari hayo kutoka Korea wanaotokana na Shirika la Kimataifa la Christian Life World Mission Frontiers lenye makazi yake nchini Korea.



Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464