SHANG JIE : UHABA WA MAFUTA UTAPUNGUA TUKIONGEZA UZALISHAJI MALIGHAFI


Mkurugenzi wa Kampuni ya Jielong Holding (T) Ltd inayozalisha mafuta ya alizeti na pamba mjini Shinyanga,  Shang Jie akielezea kuhusu uzalishaji wa mafuta katika kiwanda hicho. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Muonekano wa sehemu ya mafuta ya pamba yaliyosindikwa katika Kampuni ya Jielong Holding (T) Ltd inayozalisha mafuta ya alizeti na pamba mjini Shinyanga. 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkurugenzi wa Kampuni ya Jielong Holding (T) Ltd inayozalisha mafuta ya alizeti na pamba mjini Shinyanga,  Shang Jie amewaomba wananchi kulima zao la pamba, alizeti na michikichi kwa wingi kwani mitambo ya kusindika mazao hayo ipo lakini malighafi hazitoshi.

 

Shang Jie amesema hayo Julai 15,2022 wakati Maafisa Mawasiliano wa Wizara ya Kilimo na Bodi ya Pamba Tanzania walipotembelea kiwanda hicho kilichopo Nhelegani Manispaa ya Shinyanga.

 Mwekezaji huyo kutoka China amesema kiwanda chake kina uwezo mkubwa wa kuzalisha mafuta ambapo kwa siku moja wana uwezo wa kusindika tani 350 za mbegu za mafuta ya alizeti na tani 450 za pamba lakini changamoto kubwa waliyonayo ni upatikanaji wa malighafi hali inayosababisha kiwanda kufanya kazi kwa asilimia 30 hadi 40 hivyo kuwaomba wananchi kuchangamkia fursa ya kilimo ili kupata malighafi.

Ameeleza kuwa kutokana na changamoto hiyo imesababisha wasitishe usindikaji wa mafuta ya alizeti na sasa wana mpango wa kupeleka mitambo ya kukamua mafuta ya michikichi mkoani Kigoma ili kuendelea na uzalishaji wa mafuta.

Amesema hivi sasa wanaendelea na usindikaji wa mafuta ya pamba na kuzalisha mashudu ambayo wanayasafirisha nje ya nchi huku soko la mafuta likiwa katika mikoa mbalimbali nchini. 

“Kinachotakiwa ni wananchi kuendelea kulima mazao haya kwa tija ili viwanda hivi vifanye kazi kwa uwezo wa kiwanda kwa msimu wa mwaka mzima na endapo tutapata malighafi tatizo la upatikanaji wa mafuta litapungua kwa kiasi kikubwa hapa nchini”,amesema Shang Jie.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Jielong Holding (T) Ltd inayozalisha mafuta ya alizeti na pamba mjini Shinyanga,  Shang Jie (wa tatu kulia) akielezea kuhusu uzalishaji wa mafuta katika kiwanda hicho. Kushoto ni Afisa Mawasiliano Wizara ya Kilimo, Nyabaganga Taraba akiandika dondoo muhimu.
Muonekano wa sehemu ya mafuta ya pamba yaliyosindikwa katika Kampuni ya Jielong Holding (T) Ltd inayozalisha mafuta ya alizeti na pamba mjini Shinyanga
Mbegu za pamba zikiwa ndani ya kiwanda cha Kampuni ya Jielong Holding (T) Ltd inayozalisha mafuta ya alizeti na pamba mjini Shinyanga
Mbegu za pamba zikiendelea kuchambuliwa kabla ya kusindikwa kuwa mafuta ndani ya kiwanda cha Kampuni ya Jielong Holding (T) Ltd inayozalisha mafuta ya alizeti na pamba mjini Shinyanga
Mashudu yakiwa ndani ya kiwanda cha Kampuni ya Jielong Holding (T) Ltd inayozalisha mafuta ya alizeti na pamba mjini Shinyanga.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464