MISA TANZANIA YAKUTANA NA WAHARIRI...KWAYU ATAKA MSUKUMO MABADILIKO YA SHERIA

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Brain Incorperated Ltd, Jesse Kwayu akitoa mada kuhusu sheria mbalimbali za vyombo vya habari kwenye semina kwa Wahariri wa Habari iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA leo Ijumaa Julai 8,2022 jijini Dar es salaam.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Brain Incorperated Ltd, Jesse Kwayu amewataka waandishi wa habari nchini Tanzania kuungana na kuendelea kusukuma mabadiliko ya vifungu mbalimbali vya sheria zinazosimamia taaluma ya uandishi wa habari,ambavyo vinaminya utendaji na ukuaji wa vyombo vya habari.

Aidha, amewataka kuzisoma mara kwa mara sheria hizo,kutoa maoni yao kwenye mchakato wa mabadiliko uliopo sasa,kwani kwa kufanya hivyo ni kuonyesha kujali na kwa kiasi gani jambo linawagusa.

Kwayu ametoa rai hiyo leo Ijumaa Julai 8,2022 Jijini Dar es salaam wakati wa Semina kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari kuhusu sheria mbalimbali za habari za vyombo vya habari nchini Tanzania, yaliyoandaliwa na Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Jangwa la Sahara (Media Institute of Southern Africa,Tawi la Tanzania (MISA Tanzania) kwa Kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake nchini (TAMWA) kupitia Mradi wa International Media Support - IMS.

Semina hiyo ililenga kuwajengea uwezo Wahariri wa Habari kutambua na kuchambua sheria hizo pamoja na kutoa maoni yao.

Kwa mujibu wa Kwayu, baadhi ya vifungu vya Sheria ya Huduma za Habari , Sheria ya Takwimu na Sheria ya Udhibiti wa Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA), zinaminya uhuru wa kujieleza, upatikanaji wa taarifa na ukuaji wa vyombo vya habari nchini na kwamba zinahitaji kufanyiwa marekebisho ili kuwa rafiki kwa maendeleo ya nchi.

"Ukishakuwa na sheria mbaya huwezi jua saa ngapi itakukamata. Tusilale tusome, tupige kelele kuhusu sheria zinazotukandamiza, hizi sheria bado hazijarekebishwa,tupo kwenye mchakato ambao ni lazima tushiriki kwa kuwa inatuhusu,"amesema.

"Sheria hizi zina mamlaka makubwa sana, mfano Sheria ya EPOCA ni kubwa , inatugusa katika maisha yetu ya kila siku, kelele za kufanyia marekebisho sheria hii ziendelee kila siku. Tuna wajibu wa kupaza sauti kujitetea wenyewe juu ya sheria hizo ili pale inapowezekana ziweze kufanyiwa marekebisho ili zisiwe mwiba kwa wanahabari na vyombo vya habari", ameongeza Kwayu.

Katika hatua nyingine Kwayu amewasisitiza waandishi wa habari kuwa mstari wa mbele kutetea haki zao na kutetea za wananchi katika jamii, kwa kuwa wengi wamezikosa kwa kutozitambua jambo ambalo siyo sahihi.

“Waandishi wa habari ni watetezi wa haki za binadamu. Jambo linaloumiza mtu wewe mwandishi wa habari lazima likukere . Kama mwandishi wa habari hukereketwi na jambo la jamii achana na kazi ya uandishi wa habari kafanye kazi nyingine,ni lazima mjisimamie na kuwa tayari kusaidia mtu au jamii inapoumizwa”,amesema Kwayu ambaye alikuwa Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Nipashe.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa TAMWA, Dkt. Rose Reuben amewataka waandishi wa habari kuona umuhimu wa kuzingatia utekelezaji wa masuala ya jinsia kwa kuzingatia masuala ya usawa wa kijinsia wanapoandika habari zao.

"Huku kwenye vyombo vya habari tuweke kipaumbele kwenye masuala ya kijinsia na habari tunazoziandika zizingatie masuala ya jinsia",amesema Dkt. Reuben.

Nao washiriki wa semina hiyo akiwemo Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa Shirika la Habari Ujerumani (DPA) Peter Nyanje na Mwandishi wa habari Mwandamizi kutoka TBC, Chilu Matuzya wameishukuru MISA- Tanzania kwa kutoa mafunzo hayo huku wakishauri madawati ya jinsia kuanzishwa kwenye vyombo vya habari na kuhakikisha habari za kijinsia zinapewa kipaumbele.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Brain Incorperated Ltd, Jesse Kwayu akitoa mada kuhusu Haki na Uhuru wa Kujieleza kwenye semina kwa Wahariri wa Habari iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA leo Ijumaa Julai 8,2022 jijini Dar es salaam. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Brain Incorperated Ltd, Jesse Kwayu akitoa mada kuhusu sheria mbalimbali za vyombo vya habari kwenye semina kwa Wahariri wa Habari iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Brain Incorperated Ltd, Jesse Kwayu akitoa mada kuhusu sheria mbalimbali za vyombo vya habari kwenye semina kwa Wahariri wa Habari iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA leo Ijumaa Julai 8,2022 jijini Dar es salaam.
Afisa Programu kutoka MISA-TAN, Jacqueline Jones akizungumza kwenye semina kwa Wahariri wa Habari iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA
Afisa Programu kutoka MISA-TAN, Jacqueline Jones akizungumza kwenye semina kwa Wahariri wa Habari iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA
Wahariri wa Habari wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA.
Wahariri wa Habari wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA
Mkurugenzi wa TAMWA, Dkt. Rose Reuben akitoa mada kuhusu masuala ya kijinsia kwenye semina kwa Wahariri wa Habari iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA
Mkurugenzi wa TAMWA, Dkt. Rose Reuben akitoa mada kuhusu masuala ya kijinsia kwenye semina kwa Wahariri wa Habari iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA
Mshauir wa Vyombo vya Habari/ Mkufunzi, Rose Haji Mwalimu akizungumza kwenye semina kwa Wahariri wa Habari iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA
Mwenyekiti wa MISA - Tanzania , Salome Kitomari akizungumza wakati wa semina kwa wahariri wa habari kuhusu sheria mbalimbali zinazohusu tasnia ya habari
Wahariri wa Habari wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA
Wahariri wa Habari wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA.
Wahariri wa Habari wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA.
Esther Zelamula kutoka Channel Ten akichangia hoja kwenye semina hiyo.
Jennifer Sumi kutoka AZAM Media akichangia hoja wakati wa semina hiyo
Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa Shirika la Habari Ujerumani (DPA) Peter Nyanje akichangia hoja kwenye semina hiyo
Mhariri kutoka Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Nicodemus Ikonko akichangia hoja kwenye semina hiyo
Mwandishi wa habari Mwandamizi kutoka TBC, Chilu Matuzya akichangia hoja wakati wa semina hiyo.
Mhariri wa Habari Gazeti la Jamhuri, Dennis Luambano akichangia hoja kwenye semina hiyo
Wahariri wa Habari wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA.
Wahariri wa Habari wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA.
Wahariri wa Habari wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA.
Wahariri wa Habari wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA.
Wahariri wa Habari wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA.
Wahariri wa Habari wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA.
Wahariri wa Habari wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA.
Wahariri wa Habari wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464