MWENGE WA UHURU WAZINDUA NA KUWEKA MAWE YA MSINGI MIRADI YA MAENDELEO MANISPAA YA SHINYANGA


Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, mwaka 2022 Sahili Nyanzabara Geraruma akiweka Jiwe la Msingi katika Shule ya Msingi Bugweto Manispaa ya Shinyanga mara baada ya kukagua vyumba Sita vya Madarasa Ofisi mbili za walimu, (kushoto) ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (kulia) ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma, amezindua na kuweka mawe ya Msingi kwenye Miradi ya Maendeleo Manispaa ya Shinyanga, na kushiriki ujenzi wa Jengo la Utawala Manispaa ya Shinyanga.

Mwenge huo wa Uhuru umekimbizwa leo Julai 27,2022 katika Manispaa ya Shinyanga, ukitokea halmashauri ya Shinyanga, ambao umepitia Miradi Mitano ya Maendeleo na yote imekubaliwa.

Akizungumza wakati akikagua Miradi hiyo ya maendeleo kwa nyakati tofauti, Geraruma amesema Miradi yote ni mizuri na ameridhia kuweka Mawe ya Msingi pamoja na kuizindua.

"Miradi yote ya maendeleo ambayo nimeipitia ni mizuri na ile ambayo nimetoa maelekezo ifanyiwe marekebisho na kuendelea kutoa huduma bora kuwa wananchi," amesema Geraruma.

Katika hatua nyingine, ametoa wito kwa wananchi wa Shinyanga siku ya Kuhesabiwa Sensa ya watu na Makazi itakayofanyika Agosti 23 mwaka huu, wajitokeze kwa wingi kuhesabiwa.

Naye Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana Ajira na Wenye ulemavu, amepongeza usimamizi mzuri wa Miradi hiyo ya maendeleo na kutumia fedha vizuri ambazo zimetolewa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Rajab Masanche, awali akipokea Mwenge huo wa Uhuru kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Nice Munissy amesema Mwenge huo utazindua Miradi ya maendeleo Miwili ambayo ni Ujenzi wa Zahanati ya Shushu na Mradi wa Maji Bugwandege.

Amesema Mwenge huo pia umeweka Mawe ya Msingi katika Kiwanda cha Bia cha Gaki Investment, ujenzi vyumba vya Madarasa Sita na Ofisi mbili za walimu katika Shule ya Msingi Ugweto. Pia Mwenge huo ulipita kwenye viwanja vya Mazingira Center.

Kauli Mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka huu (2022) inasema "Sensa ni Msingi wa Mipango ya Maendeleo, Shiriki kuhesabiwa kwa Maendeleo ya Taifa.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma, akizungumza wakati wa uzinduzi na uwekaji mawe ya msingi kwenye miradi ya maendeleo iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu, akizungumza kwenye ufunguzi na uwekaji mawe ya msingi kwenye miradi iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye Mbio za Mwenge wa Uhuru Manispaa ya Shinyanga.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (kushoto) akiteta jambo na Kiongozi wa Mbizo za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma, katika Zahanati ya Bushushu.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma, akiweka jiwe la Msingi na kuzindua Zahanati ya Bushushu,
(kushoto ) ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (kulia) ni Mbunge wa Jimbo la Shinanga Mjini Patrobas Katambi.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma, akiweka jiwe la Msingi na kuzindua Mradi wa Maji katika kijiji cha Bugwandege Manispaa ya Shinyanga uliotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA).

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma, akiwa katika kiwanda cha uzalishaji Bia cha Gaki Investment.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma, akweka Jiwe la Msingi katika kiwanda cha Bia Gaki Investment.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, mwaka 2022 Sahili Nyanzabara Geraruma akiweka Jiwe la Msingi katika Shule ya Msingi Bugweto Manispaa ya Shinyanga mara baada ya kukagua vyumba Sita vya Madarasa Ofisi Mbili za walimu, (kushoto) ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (kulia) ni Mbunge wa Jimbo la Shinanga Mjini Patrobas Katambi.

Muonekano wa vyumba sita vya madarasa katika Shule ya Msingi Bugweto.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma, akishiriki ujenzi wa Jengo la Utawala la Manispaa ya Shinyanga.

Ujenzi ukiendelea wa Jengo la Utawala Manispaa ya Shinyanga.

Muonekano wa picha Jengo la Utawala la Manispaa ya Shinyanga jinsi litakavyokuwa.

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Rajab Masanche, akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Nice Munissy (kushoto) kwa ajili ya kuukimbiza katika Manispaa hiyo na kuzindua na kuweka mawe ya msingi miradi ya maendeleo.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiushika Mwenge wa Uhuru na kuupokea katika Manispaa ya Shinyanga.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu, akiushika Mwenge wa Uhuru.

Mbunge wa Vitimaalum Ruthi Mayenga akishika Mwenge wa Uhuru na kuupokea katika Manispaa ya Shinyanga.

Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akiushika Mwenge wa Uhuru.

Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Ester Makune akiushika Mwenge wa Uhuru.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464