UGONJWA ULIOIBUKA LINDI NI HOMA YA MGUNDA

Upimaji wa sampuli za wagonjwa waliokuwa wakiugua ugonjwa usiojulikana katika Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi umethibitisha mlipuko huu kuwa wa ugonjwa wa homa ya Mgunda ‘Leptospirosis, Field Fever’.

Hayo yamejulikana ikiwa ni siku nne zimepita tangu Serikali ya Tanzania ikubali ombi la Shirika la Afya Duniani (WHO) na Kituo cha kukinga na kudhibiti magonjwa (CDC) kutoka Serikali ya Marekani kuongeza nguvu kwenye timu ya wataalamu katika kubaini ugonjwa huo.

Akizungumza leo Jumatatu, Julai 18, 2022 Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametoa taarifa hiyo baada ya kutembelea Wilaya ya Ruangwa katika Mkoa wa Lindi ambako kumezuka mlipuko huo.


 SOMA ZAIDI HAPA CHANZO MWANANCHI.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464