WAJUMBE BODI YA MAJI SHUWASA WATEMBELEA MIRADI YA MAJI FEDHA ZA UVIKO-19, WAPONGEZA KASI UTEKELEZAJI WA MIRADI HIYO

Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) wakiwa katika mradi wa maji kwenye kijiji cha Magwata Manispaa ya Shinyanga, wakishuhudia maji yakitoka bombani na kuhudumia wananchi.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

WAJUMBE wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) wametembelea miradi ya maji ambayo imetekelezwa na Mamlaka hiyo, kupitia fedha za mkopo za kukabiliana na athari za UVIKO-19.
 
Mamlaka hiyo ya Maji (SHUWASA) ilipokea fedha za UVIKO-19, Sh.milioni 469. kwa ajili ya kutekeleza miradi ya Maji safi na salama kwa wananchi, na kuwaondolea adha ya ukosefu wa maji katika maeneo yao, pamoja na kuacha kutumia maji yasiyofaa kwa matumizi ya binadamu.

Wajumbe hao wa Bodi ya Maji (SHUWASA), wamefanya ziara hiyo leo Julai 14,2022, wakiwa wameambatana na Menejimenti ya Mamlaka hiyo, kwa kutembelea miradi ya maji ya fedha za UVIKO-19, katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na Manispaa ya Shinyanga.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo ya Maji Shinyanga (SHUWASA) Mwamvua Jilumbi, ameipongeza Menejimenti ya (SHUWASA), kwa kutekeleza miradi hiyo ya Maji ya fedha za UVIKO-19, kwa wakati na kiwango kinachotakiwa.

Amesema awali walipokuwa wakiwaeleza Bodi kuwa miradi hiyo ya Maji ya fedha hizo za UVIKO-19, kuwa hadi kufikia Juni mwaka huu itakuwa imeshakamilika hawakuamini, lakini leo wameshuhudia wenyewe maji yakitoka bombani na kuhudumia wananchi.

"Tunaipongeza Menejimenti ya (SHUWASA), kwa kukamilisha Miradi hii ya Maji kwa wakati itokanayo na fedha za UVIKO-19, awali hakuamini lakini mmetudhihirishia kazi mnaiweza na maji yanatoka bombani," amesema Jilumbi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo ya Majisafi na usafi wa Mazingira Shinyanga(SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola, amesema walipopokea fedha hizo za UVIKO-19, walizielekeza kutekeleza miradi ya maji kwenye maeneo ya pembezoni ambayo hayakuwa na huduma kabisa ya maji safi na salama.

Ametaja maeneo hayo kuwa ni Kijiji cha Bugwandege, Magwata, Bugimbagu vyote vya Manispaa ya Shinyanga, na vijiji vya Didia na Iselamagazi wilayani Shinyanga na miradi hiyo inatoa huduma ya maji kwa wananchi.

"Fedha ambazo tulipokea za mkopo wa mapambano ya athari ya UVIKO-19 ni Sh.milioni 469.8 na tumetumia milioni 406 na imebaki Sh.milioni 63, fedha ambazo tunasubiri maelekezo ya Wizara ya Maji tuzifanyie kitu gani," amesema Katopola.

Nao baadhi ya wananchi ambao wamepata huduma hiyo ya Majisafi na salama, wameishukuru Serikali kwa kutekeleza miradi ya maji maeneo yao, ambayo imewaondolea changamoto mbalimbali zitokanazo na ukosefu wa Maji.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mwamvua Jilumbi akizungumza walipotembelea miradi ya Maji ya fedha za UVIKO-19.

Mkurugenzi wa Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola akizungumza kwenye ziara hiyo ya Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka hiyo.

Mkurugenzi wa Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola, akielezea namna walivyotekeleza Miradi ya Maji itokanayo na fedha za UVIKO-19.

Mkurugenzi wa Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola, akielezea namna walivyotekeleza Miradi ya Maji itokanayo na fedha za UVIKO-19.

Kaimu Meneja ufundi wa (SHUWASA) Mhandisi Uswege Mussa ambaye pia ni Meneja usambazaji Maji, akizungumza kwenye ziara hiyo ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi.

Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Maji (SHUWASA) wakiwa katika mradi wa maji katika kijiji cha Bugwandege Kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.

Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Maji (SHUWASA) wakiwa katika Mradi wa Maji katika kijiji cha Magwata Kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Maji (SHUWASA) Mwamvua Jilumbi, akikagua ubora wa sakafu katika mradi wa maji katika kijiji cha Magwata Kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga .

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola (kulia) akiwa na Mtumishi wa Mamlaka hiyo Mwandumbya, wakiwa katika Tenki la kuhifadhia Maji, Kata ya Didia wilayani Shinyanga.
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji (SHUWASA) wakiendelea na ziara ya kutembelea miradi ya maji itokanayo na fedha za UVIKO-19.

Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji (SHUWASA) wakiendelea na ziara ya kutembelea miradi ya maji itokanayo na fedha za UVIKO-19.

Baaadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Maji Shinyanga (SHUWASA) wakiwa kwenye ziara ya Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka hiyo.

Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji Shinyanga (SHUWASA) wakiendelea na ziara ya kutembelea miradi ya maji itokanayo na fedha za UVIKO-19.

Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji Shinyanga (SHUWASA) wakiwa katika Ujenzi wa Tenki la Mradi wa Maji Tinde kwenda Shelui.

Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji Shinyanga (SHUWASA) wakiwa na baadhi ya watumishi wa Mamlaka hiyo katika Ujenzi wa Tenki la Mradi wa Maji Tinde kwenda Shelui.

Ziara ikiendelea ya kutembelea miradi ya maji ambayo imetekelezwa na fedha za UVIKO-19.

Ziara ikiendelea ya kutembelea miradi ya maji ambayo imetekelezwa na fedha za UVIKO-19.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464