WFT-Trust WAFUNGA MRADI WILAYANI SHINYANGA, UKATILI WAPUNGUA, SERIKALI YATENGA BAJETI MAPAMBANO UKATILI WANAWAKE NA WATOTO


Mratibu wa Mfuko wa Ruzuku wa Wanawake Tanzania (WFT-Trust) mkoani Shinyanga Glory Mbia, akizungumza kwenye kikao cha kufunga mradi.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MFUKO wa Ruzuku wa Wanawake Tanzania (WFT-Trust) umefunga Rasmi Mradi wa kupinga matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto uliokuwa ukitekelezwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Mradi huo umefungwa leo Julai 28, 2022 katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau wa maendeleo kutoka mashirika mbalimbali, Taasisi na vyombo vya habari ambavyo vilikuwa vikitekeleza mradi huo.

Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Deus Mhoja, amesema mradi huo umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya Wanawake na Watoto katika Halmashauri hiyo.

Amesema Serikali itaendelea kushirikia na wadau mbalimbali wa maendeleo katika Halmashauri hiyo ya wilaya ya Shinyanga, ili kuhakikisha jamii kubaki salama.

“Katika kuunga juhudi za wadau za mapambano dhidi ya kupinga ukatili wa wanawake na watoto, Idara yetu ya Maendeleo ya jamii katika mwaka wa fedha (2022-2023) tumetengewa kiasi cha fedha Sh.milioni 20 ambazo zitatumika kuendelea mapambano haya,”amesema Mhoja.

“Fedha hizi pia zitatumia kuunda Mabaraza ya Watoto, Majukwaa ya Wanawake, kutengeneza mfumo utakaosaidia kupata takwimu sahihi za matukio ya ukatili wa kijinsia kwa kushirikisha wadau,”ameongeza.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ya wilaya ya Shinyanga David Rwazo, amewapongeza wadau waliopata fedha za ufadhili kutoka (WFT-Trust) kuwa wametendea haki fedha hizo la kuleta matokeo chanya na kupunguza matukio ya ukatili wa kijinsia ndani ya jamii.

Kwa upande wake Mratibu wa Mfuko wa Ruzuku wa Wanawake Tanzania (WFT-Trust) mkoani Shinyanga Glory Mbia, ameshukuru wadau kwa kazi yao kubwa walioifanya ya kupunguza ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Aidha, amekazia ushauri ambao umetolewa na wajumbe kwenye kikao hicho, kuwa shughuli kama hizo za kupambana kupinga matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto ziwe zinaingizwa kwenye mipango ya Bajeti ya Halmashauri, na siyo kutegemea fedha za wafadhili pekee.

Mashirika ambayo yalipata ufadhili wa fedha kutoka (WFT-Trust) na kutekeleza mradi huo wa mapambano ya kupinga ukatili wa wanawake na watoto Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ni Rafiki-SDO, YAWE, WEADO, THUBUTU, AGAPE, GCI, Klabu ya waandishi wa Habari mkoani Shinyanga.

Wengine ni Radio Faraja, Dawati la Jinsia kutoka Jeshi la Polisi, pamoja na Halmashuri ya wilaya ya Shinyanga, ambapo mradi huo ulitekelezwa kwa muda wa miezi sita kuanzia Januari hadi June mwaka huu kwa awamu awamu.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ya wilaya ya Shinyanga David Rwazo akizungumza kwenye kikao hicho cha kufunga Mradi.

Pastory Mfoi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akizungumza kwenye kikao hicho.

Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Deus Mhoja akizungumza kwenye kikao hicho.

Mratibu wa Mfuko wa Ruzuku wa Wanawake Tanzania (WFT-Trust) mkoani Shinyanga Glory Mbia, akizungumza kwenye kikao cha kufunga mradi.

Mratibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Shinyanga Estomine Henry akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi wa kupinga ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Mratibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Shinyanga Estomine Henry akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi wa kupinga ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Mariamu Maduhu kutoka Shirika la Rafiki-SDO akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi wa kupinga ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Winie Hinaya Shirika la WEADO akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi wa kupinga ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Pascharia Mbugani kutoka Shirika la Thubutu Afrika Intiatives akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi wa kupinga ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Deus Lyakisi kutoka Shirika la YAWE akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi wa kupinga ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Dawati la Polisi wilaya ya Shinyanga wakiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi wa kupinga ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Getruda Thomas kutoka Radio Faraja akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa kupinga ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Mkurugenzi wa Shirika la AGAPE John Myola akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa kupinga ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Aisha Omary akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa kupinga ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Waandishi wa Habari Mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao hicho cha kufunga mradi wa (WFT-Trust) wa kupinga ukatili dhidi ya Wanawake na watoto Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Waandishi wa Habari Mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao hicho cha kufunga mradi wa (WFT-Trust) wa kupinga ukatili dhidi ya Wanawake na watoto Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Waandishi wa Habari Mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao hicho cha kufunga mradi wa (WFT-Trust) wa kupinga ukatili dhidi ya Wanawake na watoto Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Waandishi wa Habari Mkoani Shinyanga wakiwa kwenye kikao hicho cha kufunga mradi wa (WFT-Trust) wa kupinga ukatili dhidi ya Wanawake na watoto Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Mratibu wa (WFT-Trust) mkoani Shinyanga Glory Mbia (kulia) akiwa na Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Aisha Omary kwenye kikao hicho.

Kikao kikiendelea

Mtendaji wa Kata ya Pandagichiza wilayani Shinyanga Deogratius Mashamba akiwa kwenye kikao hicho.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Picha ya pamoja ikipigwa kwenye kikao hicho.

Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.

Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464