Na Kareny Masasy
WAZAZI na walezi wa manispaa ya Shinyanga wameaswa kuachana na tabia ya kuwafunga watoto kama wanyama bali wawe wanawalea kwenye kutazama malezi zaidi wawapo majumbani.
Hayo yamesemwa leo tarehe 21/08/2022 na askofu David Mabushi wa Kanisa la International Evangelical Assemblies of God Tanzania,lililopo manispaa ya Shinyanga katika ibada ya jumapili,wakati akitoa mahubiri kwa maandalizi ya wiki ya watoto kwa kanisa hilo.
Mabushi amesema wazazi na walezi wamekuwa na tabia ya kuwafanya watoto kama mifugo na kutowalea kwa msingi bora ya kidini na malezi yaliyo muhimu ya jamii matokeo yake wamejikita kufuatilia chakula na malazi tu.
Mabushi amesema wazazi hawana muda na watoto na badaye kuwalaumu kuwa kizazi cha siku hizi kina shida,jukumu la wazazi ni kufatilia mwenendo wa watoto na kuwapa adhabu zinazostahili ili waondokane na ujinga na matendo maovu yasiyofa kwa Mungu na jamii.
"Tuna mchango gani kwa watoto wetu kama hatuweki muda wa kufatilia tabia na mienendo yao,tuko bize na kuwatafutia chakula na malazi kama mifugo tu,tunawafanya watoto kuwa mifugo na hakuna muda wa majadiliano na kufundishana maadili ya dini na jamii"
Kwa upande wake,Mama mchungaji wa kanisa hilo,Suzani Mabushi amesema mikoa ya kanda ya ziwa baadhi ya wazazi na walezi hawana msukumo wa kupeleka watoto shule na kuwapatia mafunzo ya dini, ukilinganisha na mikoa ya kasikazini.Pia wazazi na walezi wa kanda ya ziwa wanaona mafunzo ya dini sio lazima.
"Watoto tukae nao wenyewe wajue hali ya mzazi ikoje kwa mazingira yoyote tusiwapeleke wakakaa hovyo ndugu wengine sio watu wazuri" anasema suzani.
Ngatale Peter muumini wa kanisa hilo amesema kuwa changamoto iliyopo kwa sasa ya kuwalea watoto hovyo ni jambo linalosababisha kuwepo na athari za vitendo vya ukatili ni vyema kuwakumbuka watoto katika malezi.
mwisho.