FADev YAKUTANA NA WANAHABARI, WAHARIRI KUJADILI NAMNA YA KUMUENDELEZA MCHIMBAJI MDOGO WA MADINI


Katibu Mtendaji wa Taasisi ya kuendeleza Uchimbaji mdogo wa Madini FADev Mhandisi Theonestina Mwasha, akizungumza kwenye Semina hiyo.

Na Marco Maduhu, MWANZA

TAASISI ya kuendeleza Uchimbaji mdogo Madini  FADev, imeendesha Semina ya siku mbili kwa Wanahabari na Wahariri kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa, kujadili namna ya kumuendeleza mchimbaji mdogo wa madini.

Semina hiyo imeanza kufanyika leo Jijini Mwanza Agosti 30, 2022, na itahitimishwa kesho Agosti 31.

Katibu Mtendaji wa FADev Mhandisi Theonestina Mwasha, amesema lengo la Semina hiyo ni kujadiliana na kuona namna ya kumuendeleza mchimbaji mdogo wa madini, pamoja na kuandika taarifa ambazo zitawakuza na pia kuongeza pato lao na Taifa kwa ujumla.

"Taasisi ya FADev tunaunga juhudi za Serikali katika kukuza Sekta ya uchimbaji mdogo wa madini hapa nchini, na tumekuwa tukikutana na wadau mbalimbali kujadili changamoto ambazo zinawakabili wachimbaji wadogo na kuzitafutia ufumbuzi," amesema Mwasha.

Aidha, amesema mbali na kukutana na wadau mbalimbali, pia wamekuwa wakisaidia wachimbaji wadogo wa Madini, kuwapatia huduma za kitalaam za kifedha, pamoja na kuwaonyesha na kuwaunga kwenye Taasisi za kifedha ili wapate mikopo na kukuza mitaji yao.

Kwa upande wake Meneja Program na utafiti kutoka FADev Evans Rubara, amesema dhima ya Taasisi hiyo ni kuona Sekta ya uchimbaji mdogo wa madini  ina kuwa jumuishi, na endelevu.

Amesema pia katika vipengele vyao vitano, ni kuona Sekta ya Uchimbaji mdogo wa Madini ina rasimishwa, shughuli za uchimbaji zinafuata kanuni za utunzaji wa Mazingira, wanawake wanashiriki kikamilifu, wachimbaji wafanye shughuli zao kibiashara zaidi, pamoja na kufanya majadiliano endelevu na wadau.

Katika hatua nyingine, amewataka Wanahabari wawe wanaandika taarifa za mara kwa mara ambazo zinahusu Sekta hyo ya uchimbaji mdogo wa madini.

Katibu Mtendaji wa Taasisi ya kuendeleza Uchimbaji mdogo wa Madini FADev Mhandisi Theonestina Mwasha, akizungumza kwenye Semina hiyo.

Katibu Mtendaji wa Taasisi ya kuendeleza Uchimbaji mdogo wa Madini FADev Mhandisi Theonestina Mwasha, akizungumza kwenye Semina hiyo.

Meneja Program na utafiti kutoka FADev Evans Rubara, akizungumza kwenye Semina hiyo.

Meneja Program na utafiti kutoka FADev Evans Rubara, akizungumza kwenye Semina hiyo.

Dk. Abel Kinyondo akizungumza kwenye Semina hiyo.

Wahabari na Wahariri wakiwa kwenye Semina ya Taasisi ya kuendeleza uchimbaji mdogo wa madini FADev.

Semina ikiendelea.

Semina ikiendelea.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464