KIKOSI KAZI CHA MAHAKIMU KUMALIZA MRUNDIKANO WA MASHAURI MAHAKAMANI WATUNUKIWA VYETI VYA PONGEZI


Hakimu wa Mahakama ya Meatu Mohamed Richard ambaye ni miongozi mwa kikosi kazi cha Mahakimu wa kumaliza mrundikano wa Mashauri Mahakamani akipokea Cheti cha Pongezi kutoka kwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Athumani Matuma.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MAKAHAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga ambayo ina hudumia na Mkoa wa Simiyu, imewatunuku vyeti vya pongezi kikosi kazi cha Mahakimu Sita ambao walijitolea kushughulikia mrundikano wa Mashauri Mahakamani.

Hafla hiyo ya kutunuku vyeti hivyo vya pongezi kwa Mahakimu hao pamoja na Maofisa Tawala wawili wa Mahakama ya wilaya ya Kahama na Kishapu na Mkuu wa Mashitaka mkoani Simiyu, imefanyika leo Agosti 26, 2022 katika viwanja vya Makahama kuu Kanda ya Shinyanga.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Athumani Matuma, amesema walikaa na kubuni mbinu namna ya kupunguza mrundikano wa Mashauri Mahakamani, ndipo wakaunda kikosi kazi hicho cha Mahakimu, ambao wanafanya kazi ya kujitolea kutembelea Mahakama za wilaya na Mkoa kupunguza Mrundikano wa Kesi.

“Kikosi kazi hiki tumekiunda mwaka huu, lakini ndani ya muda mfupi kimeleta matunda na kupunguza mrundikano wa Mashauri Mahakamani, na leo tunawatunuku vyeti vya pongezi kutokana na kazi kubwa ambayo wameifanya,”amesema Jaji Matuma.

“Licha ya kuwa na kikosi hiki kazi kutembelea katika Mahakama za Wilaya na Mkoa kushughulikia mrundikano wa Mashauri, na sisi hapa Mahakama kuu Kanda ya Shinyanga tulikuwa na kikosi chetu, na kati ya Mashauri 56 tumeshughulikia 46 na kubaki 10,”ameongeza

Amesema pia katika kupunguza mrundikano wa Mashauri Mahakamani, wamejiwekea mikakati kuwa Katika Mahakama za Mwanzo Mashauri yasizidi Miezi Mitatu, Wilaya ya Mkoa Miezi Sita Mahakama Kuu miezi 12.

Naye kiongozi wa kikosi kazi cha Mahakimu hao Mohamed Richard, amesema walianza kushungulikia mrundikano wa Mashauri katika Mahakama ya wilaya ya Bariadi na kusikiliza kesi 43, Mahakama ya wilaya ya Maswa kesi 11 na kumaliza mrundikano wa kesi kwenye Mahakama hizo.

Amesema kikosi cha hicho kitakuwa endelevu kwa kuendelea kushughulikia mrundikano wa Mashauri Mahakamani, ili kuhakikisha wananchi wanatendewa haki kwa muda mfupi, na kueleza kuwa kwa Mahakama kuu Shauri linapaswa kukaa mwisho miaka miwili, Mkoa mwaka Mmoja na Wilaya miezi Sita.

Aidha, Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya Jinai hapa nchini Ramadhani Kingai, amesema katika kuimarisha haki, vipaumbele vya Serikali ni kupunguza mrundikano wa Mashauri Mahakamani yakiwamo ya jinai na kupunguza uhalifu hapa nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP) Antony Mwakitalu, amepongeza Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga kwa ubunifu huo, na kubainisha kuwa bila haki hakuna Amani wala Maendeleo, na kueleza kuwa Ofisi yao itakuwa ikipeleka mashitaka yaliyokamilika ili mashauri yamalizike kwa wakati.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, amesema ushughulikiaji wa mrundikano wa Mashauri Mahakamani ndiyo kiu kubwa ya Watanzania, na kukipongeza kikosi kazi hicho cha Mahakimu kwa kutanguliza uzalendo.

Mahakimu waliotunukiwa vyeti vya pongezi ni Mohamed Richard, Christiani Rugumila, Christina Chovenye, Catherine Langua, Enos Misana, na Sayi Mabondo.

Wengine waliotunukiwa vyeti vya pongezi ni Afisa tawala Mahakama ya wilaya ya Kahama Boniface Fumbe, Dotto Mabula Afisa tawala wa Mahakama ya Kishapu, na Mkuu wa Mshitaka Mkoa wa Simiyu Chema Maswi.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akizungumza kwenye hafla hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Yahaya Nawanda akizungumza kwenye hafla hiyo.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Athumani Matuma akizungumza kwenye hafla hiyo Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP) Anthony Mwakitalu akizungumza kwenye hafla hiyo.

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini Ramadahani Kingai akizungumza kwenye hafla hiyo.

Kiongozi wa kikosi kazi cha Mahakimu Sita wa kupunguza Mashauri Mahakamani Mohamed Richard akisoma Risala kwenye hafla hiyo.

Muonekano wa Jengo la Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga.

Mahakimu wakiwa kwenye hafla hiyo.

Hafla ikiendelea.

Hafla ikiendelea.

Hafla ikiendelea.

Hafla ikiendelea.

Hafla ikiendelea.

Hafla ikiendelea.

Hafla ikiendelea.

Hafla ikiendelea.

Hakimu wa Mahakama ya Meatu Mohamed Richard ambaye ni miongozi mwa kikosi kazi cha Mahakimu wa kumaliza mrundikano wa Mashauri Mahakamani akipokea Cheti cha Pongezi kutoka kwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Athumani Matuma.

Zoezi la kutunuku vyeti ya Pongezi kwa Mahakimu wa kikosi kazi cha kumaliza mrundikano wa Mashauri Mahakamani likiendelea.

Zoezi la kutunuku vyeti ya Pongezi kwa Mahakimu wa kikosi kazi cha kumaliza mrundikano wa Mashauri Mahakamani likiendelea.

Zoezi la kutunuku vyeti ya Pongezi kwa Mahakimu wa kikosi kazi cha kumaliza mrundikano wa Mashauri Mahakamani likiendelea.

Zoezi la kutunuku vyeti likiendelea.

Zoezi la kutunuku vyeti likiendelea.

Zoezi la kutunuku vyeti likiendelea.

Zoezi la kutunuku vyeti likiendelea.

Zoezi la kutunuku vyeti likiendelea.

Picha ya pamoja ikipigwa mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kutunuku vyeti Mahakimu wa kikosi kazi cha kumaliza mrundikano wa Mashauri Mahakamani.

Picha ya pamoja ikipigwa mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kutunuku vyeti Mahakimu wa kikosi kazi cha kumaliza mrundikano wa Mashauri Mahakamani.

Picha ya pamoja ikipigwa mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kutunuku vyeti Mahakimu wa kikosi kazi cha kumaliza mrundikano wa Mashauri Mahakamani.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464