KLABU YA WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA YAFANYA MDAHALO NA JESHI LA POLISI MASUALA YA ULINZI NA USALAMA, WAGUSIA KIFO CHA MWANGOSI

 
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Shinyanga (SPC) Greyson Kakuru akizungumza kwenye Mdahalo huo wa Waandishi wa Habari na Jeshi la Polisi.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

KlABU ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC), imefanya Mdahalo na Jeshi la Polisi mkoani humo kwa ajili ya kuimarisha mahusiano mazuri wakati wa utekelezaji wa majukumu yao kwa pande zote mbili na kuimarisha ulinzi na usalama kwa wanahabari.

Mdahalo huo umefanyika leo Agosti 4, 2022 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, kwa kuhusisha Waandishi wa habari pamoja na Askari wa Jeshi la Polisi.

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) Greyson Kakuru, amesema wameendesha Mdahalo huo ambao ni wapili, uliolenga kuendelea kuimarisha mahusiano mazuri ya kiutendaji kazi baina ya Waandishi wa Habari na Jeshi la Polisi, hasa wanapokutana kwenye matukio.

“Mdahalo huu ambao tunaufanya leo ni wapili, ambapo awali tuliufanya April 28 mwaka huu, na lengo kuu ni kuendelea kuimarisha mahusiano mazuri na Jeshi la Polisi na Waandishi wa Habari katika utekelezaji wa majukumu,”amesema Kakuru.

“SPC kwa kushirikiana na UTPC na IMS tutaendelea kufanya mijadala ya namna hii mara kwa mara ili kuweza kutoa elimu zaidi kwa wanahabari na Askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kupitia mradi wa ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari na kuimarisha mahusiano mazuri,”ameongeza.

Aidha, amesema kupitia mdahalo wa kwanza, tayari mafanikio yameanza kuonekana baina ya Jeshi la Polisi na Waandishi wa Habari, ambapo kumekuwa na ushirikiano mzuri hasa wanapokutana kwenye majukumu mbalimbali na kuomba mahusiano hayo yaendelee siku zote.

Katika hatua nyingine, Kakuru ametoa wito kwa Waandishi wa Habari hapa nchini kutumia vizuri kalamu zao kutoa elimu ya Sensa ya watu na makazi ili wananchi wajitokeze kwa wingi siku ya zoezi hilo ambalo liyafanyika Agosti 23 mwaka huu.

Naye Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Leonard Nyandahu, amesema jambo hilo la kufanya Mdahalo ni jema sababu linaimarisha mahusiano mazuri baina ya Jeshi la Polisi na Wanahabari na kuondoa msuguano wakati wa utekelezaji wa majukumu yao hasa wanapokutana kwenye matukio.

“Waandishi wa Habari mara nyingi tunafanya kazi za kufanana hasa kwenye masuala ya kuhabarisha umma, hivyo mdahalo huu ni mzuri sana katika kuimarisha mahusiano mazuri na kufanya kazi kwa pamoja,”amesema Nyandahu.

Naye Kaimu Afisa Polisi Jamii Mkoa wa Shinyanga Jeremiah Zitta, amewataka waandishi wa habari kuondoa mtazamo hasi juu ya Jeshi hilo kwa sababu ya kifo cha Mwandishi mwenzao Daudi Mwangosi kilichotokea Iringa mwaka 2012 , ambacho kilielezwa kilitokana na Askari Polisi, na kuomba mtazamo huo hasi uishe na kuimarisha mahusiano mazuri.

Nao Baadhi ya Waandishi wa Habari mkoani Shinyanga wakichangia mada kwenye Mdahalo huo, wameliomba Jeshi la Polisi wanapokutana kwenye matukio kila mmoja afanya kazi zake kwa mipaka ili kuondoa misuguano isiyo ya lazima, huku wakiahidi kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo.

Katika Mdahalo huo pia imeundwa Kamati ya watu Nane wakiwamo Waandishi wa Habari Wanne na Askari Polisi Wanne ambayo itakuwa ikishughulikia kutatua migogoro baina ya Wanahabari na Jeshi la Polisi.

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Shinyanga (SPC) Greyson Kakuru akizungumza kwenye Mdahalo huo.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Leonard Nyandahu akizungumza kwenye Mdahalo huo.

Kaimu Afisa Polisi Jamii Mkoa wa Shinyanga Jeremiah Zitta, akizungumza kwenye Mdahalo huo.

Katibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Shinyanga (SPC)Ally Litwayi akizungumza kwenye Mdahalo huo.

Mratibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Shinyanga (SPC) Estomine Henry akizungumza kwenye Mdahalo huo.

Mwandishi Mwandamizi Paul Mabuga akiwasilisha Mada ya usalama kwa Waandishi wa habari katika utekelezaji wa majukumu yao.

Mwandishi wa habari wa Star Tv mkoani Shinyanga Elizabert Charles akichangia Mada kwenye Mdahalo huo.

Mwandishi wa Habari Radio Kwizera mkoani Shinyanga Amosi John akichangia Mada kwenye Mdahalo huo.

Mwandishi wa habari/Mkurugenzi wa Kola Online Tv na Afisa Mahusiano wa Chuo cha Sayansi Kolandoto Josephine Charles akichangia Mada kwenye Mdahalo huo.

Mwandishi wa Habari Radio Faraja mkoani Shinyanga Simeo Makoba akichangia Mada kwenye Mdahalo huo.

Mkurugenzi wa Malunde 1 blog , Kadama Malunde akichangia Mada kwenye Mdahalo huo.

Mwandishi wa Habari wa ITV mkoani Shinyanga Frank Mshana akichangia Mada kwenye Mdahalo huo.

Mwandishi wa habari wa Nipashe Shaban Njia akichangia Mada kwenye Mdahalo huo.

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Shinyanga (SPC) Greyson Kakuru (kushoto) akiwa na Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Leonard Nyandahu, kwenye Mdahalo huo.

Waandishi wa Habari wakiwa kwenye Mdahalo.

Waandishi wa Habari wakiwa kwenye Mdahalo.

Mkurugenzi wa Malunde 1 Blog, Kadama Malunde akiwa kwenye Mdahalo.

Waandishi wa Habari wakiwa kwenye Mdahalo.

Waandishi wa Habari wakiwa kwenye Mdahalo.

Waandishi wa Habari wakiwa kwenye Mdahalo.

Waandishi wa Habari wakiwa kwenye Mdahalo.

Waandishi wa Habari wakiwa kwenye Mdahalo.
Waandishi wa Habari wakiwa kwenye Mdahalo.

Askari Polisi wakiwa kwenye Mdahalo.

Picha ya pamoja ikipigwa kwenye Mdahalo huo wa Jeshi la Polisi na Waandishi wa Habari.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464