Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizindua Medali Mbio za Shinyanga Madini Marathon.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
MBIO za Shinyanga Madini Marathon pamoja na uzinduzi wa kipindi cha Thamani ya Madini zinatarajiwa kufanyika Agosti 14 mwaka huu mkoani Shinyanga.
Katibu wa Kamati ya maandalizi Mbio za Shinyanga Madini Marathoni Roland Mwalyambi, akizungumza leo Agosti 9, 2022 wakati wa uzinduzi wa Medali, Jezi na Namba kwa ajili ya washiriki wa Mbio hizo, amesema zitafanyika katika uwanja wa CCM Kambarage.
Amesema lengo la Mbio hizo za Shinyanga Madini Marathon ni kuimarisha Afya, kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo mkoani Shinyanga, pamoja na kusaidia watoto wenye utapiamlo.
"Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema leo ametuzindulia Medali 600, Jezi na Namba za washiriki kwenye Mbio hizi, na zitakuwa za Kilomita 21, 10, 5 pamoja na Kilomita 2.5 kwa ajili ya watoto," amesema Mwalyambi.
Aidha, amesema pia kutakuwapo na Mbio za Baiskeli Kilomita 100 ,ambapo washindi wote kwenye Mbio hizo watapewa zawadi mbalimbali.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, amesema Mbio hizo za Madini Marathon zitaufungua na kutangaza Mkoa wa Shinyanga katika Sekta ya Madini na pamoja na Utalii.
Amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameshaitangaza Tanzania katika masuala ya Utalii pamoja na Madini,hivyo wataendelea kumuunga mkono kuzitangaza Rasilimali za nchi na kukuza pato la Taifa.
Kauli Mbiu ya Mbio za Shinyanga Madini Marathoni mwaka huu inasema "Kimbia kwa Afya saidia watoto wenye Utapiamlo."
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza kwenye uzinduzi wa Medali, Jezi na Namba za washiriki Shinyanga Madini Marathon.
Katibu wa Kamati ya maandalizi Shinyanga Madini Marathoni Roland Mwalyambi, akizungumza kwenye uzinduzi wa Medali, Jezi na namba za Washiriki Shinyanga Madini Marathon.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akizindua Medali za Shinyanga Madini Marathon.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akizindua Namba za Shinyanga Madini Marathon.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema (kushoto) akizindua Jezi za Shinyanga Madini Marathon (kulia) ni Katibu wa Kamati ya Maandalizi Shinyanga Madini Marathon Roland Mwalyambi. Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Shinyanga Madini Marathon Dotto Maligisa (kulia) akiwa na Katibu wake Roland Mwalyambi kwenye kikao cha maandilizi ya Mbio hizo mara baada ya kumaliza kuzindua Medali, Jezi na Namba.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao.