MBUNGE CHEREHANI AHIMIZA KILIMO CHA KIMKAKATI USHETU KWA KILA KATA


Mbunge wa jimbo  la Ushetu Emannuel Cherehani akiongea kwenye kikao  cha kawaida cha baraza la madiwani.

 Kareny  Masasy,

MBUNGE  wa jimbo la Ushetu Emanuel Charahami amewataka maafisa ushirika wasikae maofisini  badala yake kutembelea    kila  kata kutoa ushauri wa  mazao ya kimkakati ili kuongeza mapato ya halmashauri.

Mbunge Charahani amesema haya leo tarehe 25/08/2022  kwenye kikao cha kawaida cha  baraza la madiwani ambapo ameeleza kuwa  yuko tayari kugawa mbegu  bure msimu wa kilimo utakapoanza.

Charahani amesema kuwa   licha ya kuwepo kwa mazao ya kimkakati  kila kata inafahamika kwa historia ya mazao wanayolima mfano kata ya Ulowa,Ubagwe na Uyogo kilimo chao kikuu ni zao la tumbaku na  Nyankende na  Bulungwa  wao ni zao la Pamba.

Watu  wanahitaji vyama vya ushirika ili viwasaidie  kuwapa elimu na ninyi   maafisa ushirika msikae  maofisini  na  mkakati uliopo ni  kukuza    mapato ya ndani ya halmashauri badala ya kukimbizana na wajasiriamali  wadogo”amesema cherehani.

Cherehani amesema kuwa lengo la mwaka huu makadirio ni kupata kilo million 20 za pamba na  kilo Millioni 25 za zao la Tumbaku .

Kuhusiana na suala hilo madiwani wote waliunga mkono mkakati huo  ambapo   mwenyekiti wa halmashauri hiyo Lala Gaga  akipongeza  mkakati huo nakueleza ni mzuri  utaoongeza mapato ya ndani  na serikali kuu aliipongeza kwa kuleta fedha za miradi mbalimbali na kutekelezwa .

Diwani wa kata ya Nyamilangano Robert Maganga ameshauri  bakaa au fedha zinazo baki zihakikishe zinatumika kwenye robo ya mwaka inayoanza  kukamilisha miradi  iliyokuwa imelala kwa kusubiri fedha.

 Mkurugenzi wa halmashauri hiyo  Linno Mwageni amesema kuwa  ushirikiano uliopo ni mzuri atahakikisha yeye na wataalamu wenzake kusimamia vyema miradi na  kuendelea kubuni vyanzo vya mapato vipya 

Mkurugenzi wa halmashauri  ya Ushetu Linno Mwageni  akijibu hoja  katika kikao cha kawaida cha 
cha baraza la madiwani 
Madiwani wa halmashauri ya Ushetu wakisikiliza  kwa makini hoja  ya kikao.

 Mwenyekiti wa halmashauri  ya Ushetu  Gaga Lala akiahirisha  kikao cha baraza la madiwani 

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464