MCHUNGAJI WA KANISA LA KKKT,ASOMEWA SHITAKA LA KUJARIBU KULAWITI MTOTO WA MIAKA 8

 MCHUNGAJI WA KANISA LA KKKT,ASOMEWA SHITAKA LA KUJARIBU KULAWITI MTOTO WA MIAKA 8


 Mwandishi wetu,Shinyanga

 Mchungaji wa Kanisa la KKKT Makedonia Lubaga Manispaa ya Shinyanga Harold Gamalieli Mkaro amefikishwa katika Mahakama ya hakimu Mkazi Shinyanga na kusomewa Shitaka la Kujaribu Kulawiti Mtoto wa Miaka 8.

Mchungaji huyo alifutiwa kesi ya awali namba 107, August 24 na Jamhuri katika Mahakama ya Wilaya ya Shinyanga kwa sababu za Kisheria ambapo alikamatwa tena na kurejeshwa

 Mahabusu ambapo amekaa kwa muda wa siku5 hadi hii leo alipofikishwa Mahakamani tena. Akisomewa Shitaka hilo kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Shinyanga mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi Marry Mrio Mshitakiwa huyo amekana shitaka linalomkabiri la kujaribu kulawiti.

Mrio amesema kuwa Mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo la kujaribu kulawiti mtoto wa miaka 8, August 12 eneo lilipo kanisa la Makedonia Lubaga kinyume na kifungu cha 155 cha kanuni ya adhabu, sheria namba 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho 2019.

Mwendesha Mashtaka upande wa Jamhuri Jukael Jairo amesema kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekalimika na wako tayari kusoma hoja za awali na kusikiliza kesi hiyo.

Kwa upande wake wakili wa Utetezi Jeofrey Tuli ameiomba Mahakama hiyo Airisho kutokana na Mteja wake kutokuwa sawa kisaikolojia baada ya kukaa mahabusu siku5.Wakili Tulia kaomba Mteja wake kupewa dhamana na hakimu alihoji upande wa Jamhuri ambapo umesema kuwa hauna kipingamizi na dhamana iko wazi.

Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi Marry Mrio akamtaka mshitakiwa kuwa na bondi ya milioni 3 pamoja na wadhamini wawili wenye kiasi hicho hicho cha pesa pamoja na mali isiyo hamishika ambapo mmoja wa mashaihidi amekidhi vigezo na mwingine kukosa vigezo.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi kesho ambapo mahakama hiyo itaanza kuwasikiliza mashahidi sita kutoka upande wa jamahuri na Mshitakiwa amepelekwa gereza.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464