Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Kaspari Mmuya, akifuatilia zoezi la kuhesabu Sensa ya watu na Makazi Kata ya Kambarage Manispaa ya Shinyanga.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Kaspari Mmuya, ameridhishwa na zoezi la kuhesabu Sensa ya watu na Makazi katika Mikoa minne ambayo, Dodoma, Singida, Tabora na Shinyanga, na kuwatoa wasiwasi wananchi kuwa zoezi hilo ni endelevu hadi Agosti 28 na hakuna Mwananchi ambaye hatahesabiwa.
Akizungumza mara ya baada ya kuona uendeshaji wa zoezi hilo la Sensa, amesema zoezi hilo linaendelea vizuri na tangu waanze kazi ya kuhesabu majira ya saa sita usiku hakuna changamoto yoyote ambayo imejitokea hadi sasa, na wananchi wanajibu maswali vizuri ambayo wanahojiwa na Makarani na kwa ufasaha.
“Nimefarijika sana kuona zoezi hili la kuhesabu sensa ya watu na makazi lina kwenda vizuri na wananchi wanajibu maswali yote kwa ufasaha ambayo wanahojiwa, na zoezi hili ni endelevu siyo kwamba linaishia leo bali wananchi wote watahesabiwa,”amesema Mmuya.
“Kwa wale wakuu wa Kaya ambao hawatakuwepo kwenye Kaya zao ni vyema wakaacha taarifa zao vikiwamo vitambulisho na namba za simu, ili Karani akipita akute taarifa zote, na hakuna Mtanzania ambaye hatahesabiwa,”ameongeza.
Naye Mratibu wa Sensa mkoani Shinyanga Eliudi Kamendu, amesema zoezi hilo mkoani Shinyanga linakwenda vizuri, na kutoa wito kwa wananchi washiriki kikamilifu kuhesabiwa ambapo litakwenda hadi Agosti 28 mwaka huu.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Kaspari Mmuya, akizungumza mara baada ya kujionea zoezi la kuhesabu Sensa Shinyanga.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Kaspari Mmuya, akihoji Maswali kwa Mwananchi Teresia Kimondo Mkazi wa Kambarage namna zoezi hilo la Sensa linavyokwenda.
Mwananchi Teresia Kimondo Mkazi wa Kambarage akielezea namna zoezi hilo la Sensa linavyoendesha na jinsi lilivyo muhimu kwa wananchi kwa Serikali kupata idadi ya watu wake kamili kwa kila eneo.
Karani Husna Hamza Mayowana akielezea namna zoezi hilo linavyokwenda pamoja na kujibiwa maswali kwa ufasaha na wananchi.
Mratibu wa Sensa mkoani Shinyanga Eliudi Kamendu, akielezea namna zoezi hilo la Sensa mkoani humo linavyoendeshwa na kutoa wito kwa wananchi washiriki kikamilifu kuhesabiwa.