Aliyekuwa mgombea urais wa Kenya, kupitia wa Azimio la Umoja, Raila Odinga Raila, amekataa matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Agosti 9, 2022, yaliyotangazwa jana na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ya Kenya, Wafula Chebukati.
Jana, Chebukati alimtangaza mgombea urais kupitia Kenya Kwanza Dk William Ruto kuwa mshindi kwa kupata kura milioni 7.1 (asilimia 50.49) dhidi ya kura milioni 6.9 (asilimia 48.85) alizopata Odinga.
Wagombea wengine kwenye uchaguzi huo ni George Wajackoyah aliyepata kura 61,969 (asilimia 0. 44) na David Waihiga alipata kura 31,987.
Hata hivyo leo, Odinga amezungumza na waandishi wa habari na kuweka wazi kuwa hatambui matokeo hayo na hamtambui Ruto kuwa ni Rais Mteule kwasababu amepatikana kutokana na matokeo batili.
Odinga amegombea urais wa Kenya mara tano ikiwamo uchaguzi uliofanyika Agosti 9, mwaka huu na mara zote alizogombea alishindwa na wapinzani wake.
SOMA ZAIDI HAPA CHANZO MWANANCHI.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464