Na Halima Khoya, SHINYANGA
Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Mkoa Shinyanga wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuhesabiwa kwenye sensa ya watu na makazi Agost 23 mwaka huu.
Hayo yamesemwa jana na Mkuu wa Mkoa Shinyanga Bi.Sophia Mjema katika kongamano la umoja wa wanawake(UWT) lililofanyika kwenye ukumbi wa CCM Mkoa, ambapo amewataka wanawake hao kusimama imara katika zoezi la sensa pamoja na kutowaficha watoto na watu wenye ulemavu.
Hayo yamesemwa jana na Mkuu wa Mkoa Shinyanga Bi.Sophia Mjema katika kongamano la umoja wa wanawake(UWT) lililofanyika kwenye ukumbi wa CCM Mkoa, ambapo amewataka wanawake hao kusimama imara katika zoezi la sensa pamoja na kutowaficha watoto na watu wenye ulemavu.
Mjema,amewasisitiza wanawake kutoa ushirikiano wa karibu kwa makarani kwa kutoa taarifa sahihi, pamoja na kubainisha changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu, jambo ambalo litasaidia kutoa uwiano sawa kwenye huduma zitakazo tolewa na serikali.
“Ukimuelimisha Mwanamke utakua umeuelimisha Umma, na wanawake tushiriki kikamilifu kuhesabiwa Sensa pamoja na kutoa taarifa sahihi, jambo litakalo isaidia serikali kupata takwimu sahihi za watu wake na kutoa huduma stahiki kwao.”Amesema Mjema.
Kwa upande wake Mratibu wa Sensa Mkoa wa Shinyanga Eliud Kamendu, amewasihi wanawake kutoa taarifa sahihi na zinazohusu masuala ya afya ya uzazi.
Aidha, Kamendu amefafanua juu ya ya maswali aliyoulizwa na baadhi ya wanawake juu ya uwepo wa wanaume wenye kaya zaidi ya moja, amesema kuwa kutakua na usiku wa Rejea.
“usiku wa Rejea ni usiku wa kuamkia siku ya sensa tarehe 23,8,2022 ambapo kila mtu atahesabiwa pale alipolala na kwa wale wenye wake wengine watasimama kama wakuu wa kaya katika familia zao.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464