MKAGUZI MSAIDIZI WA HESABU KUTOKA TRA MKOA WA KIKODI KAHAMA HONEST MUSHI .
Na Kareny Masasy,
MSAIDIZI
mkaguzi wa hesabu kutoka mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa kikodi Kahama Honest Mushi amesema kuwa
wafanyabishara wanaamini kuwa
wasipo toa risiti malipo ya kodi
yanakuwa kidogo.
Mushi akimwakilisha meneja
wa mamlaka hiyo Warioba Kanile
katika semina ya wafanyabishara iliyofanyika leo tarehe
22/08/2022 ambayo ililenga kutoa elimu ya mabadiliko ya sheria ya ulipaji kodi kwa mwaka wa fedha wa 2022
ulioanza mwezi Julai.
“Wafanyabishara
wamekuwa wakipotoshana kuwa usipotoa risiti kodi
inakuja ndogo kitu ambacho siyo
kweli kinachotakiwa waweke rekodi za
bidhaa zao vizuri wanazouza na wahasibu
watimize wajibu wao kitu cha kwanza kwa
mfanyabiashara ni kulipa kodi”amesme Mushi .
Mushi
amesema kuwa wahasibu wamekuwa
wakiongea nao nakukosa majibu kuhusu
upigaji wa hesabu unaoleta utata ndiyo maana mamlaka ya mapato huwa inawataka
siku ya upigaji wa hesabu awepo mpiga
hesabu na mfanyabishara mwenyewe.
Mushi
amesema kuwa wapo wahasibu wazuri waliopata usajili kutoka mamlaka ya mapato na leseni
zao kila mwaka zinakwisha muda wake na
kusajiliwa upya na mfanyabiashara anatakiwa kumuandali nyaraka zote muhimu ili azifanyie kazi asipompatiwa ndiyo hapo changamoto inapotokea.
Baadhi ya
wafanyabiashara akiwemo Frank Jerome ameomba
kukombolewa kwa kupatiwa wahasibu wanaokwenda kukagua hesabu za biashara zao ili
kuendana na uhalisia wa biashara.
“ Baadhi ya
wahasibu wanakuja kuwafanyia hesabu sio
waaminifu na matokeo yake mfanyabiashara
kwenye ulipaji anaelezwa
kulipa kodi ya sh Millioni 700 sio uongo bali yupo aliyeambiwa
kiasi hicho”amesema Jerome .
Mfanyabishara Arbogast Lyimo amesema kuwa wao sio wataalamu wa mahesabu kunapotokea dosari aulizwe mtaalamu aliyepiga hesabu sababu wanakuwa wamemlipa pesa na wao kutojua chochote.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464