Na Kareny
Masasy
MAZIWA ya mama ni maalumu kwa ajili ya lishe ya mtoto, yana virutubishi vyote anavyohitaji na humkinga dhidi ya maambukizi.
Faida za
Unyonyeshaji wa maziwa ya mama unawawezesha mamilioni ya watoto wachanga na
wadogo kuishi na kuwa na maendeleo mazuri ya ukuaji.
Sheila
Mohamood anasema kuwa elimu ya unyonyeshaji mtoto baada ya kuzaliwa aliipata hospitalini
lakini amekuwa akijitahidi kunyonyesha mtoto wake ipasavyo na sasa ana
umri wa mwaka mmoja na nusu.
Pachazia
John anasema kuwa amemuachicha mtoto
wake wa mwaka mmoja ili ale na vyakula vingine
anakiri elimu ya unyonyeshaji mpaka miaka miwili ameelezwa na wataalamu
wa afya kliniki.
Samson Peter
na Musa Onesmo wanasema kuwa mtoto ni haki yake kunyonya ndiyo maana wataalamu wanawaeleza wanawake
wanyonyeshe miezi sita mfululizo bila
kumpa kitu kingine.
Ofisa
lishe halmashauri ya Msalala mkoani
Shinyanga Peter Shimba anasema kuwa unyonyeshaji wa maziwa ya
mama unaupatia nguvu mfumo wa ukuaji na maendeleo ya ufahamu na utambuzi (IQ)
wa mtoto.
Shimba anasema kwa kiasi kikubwa husaidia katika kuimarisha
mafanikio ya elimu, ushiriki katika nguvu kazi na kuongeza kipato katika maisha
ya baadaye ya mtoto.
“Wapo wazazi
ambao wamekuwa wakinga’ang’ania kuwekeza
kwa mtoto umri ambao ubongo
umekwisha komaa hauwezi tena watoto wote
wanazaliwa na akili wajitahidi kwenye unyonyeshaji”anasema Shimba
Ofisa lishe
mkoa wa Shinyanga Denis Madeleka anasema kuwa kwa mkoa wa Shinyanga una asilimia 83 ya watoto wanaonyonya maziwa
ya mama kwa kipindi cha miezi sita pekee.
Madeleka
anasema kuwa watoto wenye umri wa miezi
0 hadi 23 ni asilimia 99
walioanzishiwa maziwa ya mama ndani ya
saa moja na walioendelea kunyonya baada
ya saa moja ni asilimia 3.9.
“Waliondelea kunyonya baada ya mwaka mmoja ni
asilimia 78 wazazi wanaelezwa umuhimu wa
kunyonyesha watoto baada ya kuazaliwa na baada ya kufikisha umri wa mwaka mmoja
ikiwa wataalamu kwenye vituo vya
afya wameendelea kutoa elimu”anasema
Madeleka.
Kwa mujibu
wa Taasisi ya chakula na lishe nchini(
TFNC ) inaeleza mnamo mwaka 1990 mkutano wa wataalamu wa lishe ulifanyika nchini Italia
lengo kujadili mwelekeo wa kisera
kuhusu kuendeleza unyonyeshaji Watoto maziwa ya mama.
Mkutano huo
uliohisaniwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa ya WHO (Shirika la Afya Duniani)
na UNICEF (Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto) Ulifanyika mwaka 1990
Azimio
lililopitishwa na nchi wanachama kuweka
mazingira wezeshi kwa wanawake kuweza kunyonyesha watoto wao maziwa ya mama
pekee katika kipindi cha miezi 6 ya mwanzo .
Pia azimio
hilo limewataka wanawake kunyonyesha baada ya kujifungua na kuendelea
kuwanyonyesha watoto wao hadi watimize umri wa miaka miwili au zaidi.
Naibu Waziri
wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Mwanaidi Khamis
wakati akimwakilisha Waziri wa Afya Mhe Ummy Mwalimu anasema asilimia 97 ya watoto wanaozaliwa
hunyonyeshwa maziwa ya mama.
Naibu waziri
Khamis anasema pia asilimia 92 ya watoto
hunyonyeshwa kwa kipindi cha mwaka mmoja na kuendelea.
Naibu waziri
Khamis anasema kuwa 43% ya watoto ndio hunyonyeshwa
hadi kipindi cha miaka miwili na kuendelea .
Naibu waziri
Khamis anasema kuwa takwimu zinaonyesha
kuwa asilimia 57 ya watoto ndiyo hunyonyeshwa
maziwa ya mama pekee bila kuchanganya na chakula kingine ndani ya kipindi cha
miezi 6.
"Tafiti
zinaeleza kuwa mtoto akizaliwa na kuanza kunyonyeshwa maziwa ya mama ndani ya
saa moja kunaweza kuokoa uhai wake kwani kuchelewa kumnyonyesha mtoto kuna changia
kwa kiwango kikubwa vifo vya watoto wachanga ndani ya siku 28." anasema
Khamis .
Naibu Waziri
huyo aliwahimiza wahudumu katika vituo vya kutolea huduma za afya kutoa huduma
kwa wakati husika na kuwaasa wazazi kuendelea kuhudhuria Kliniki kama inavyoagizwa
"Kunyonyesha
maziwa ya mama kuna faida nyingi kwa mama na mtoto kwa kuwa kunaimarisha afya
na ustawi wa mama na mtoto, huzuia aina zote za utapiamlo kwa mtoto kwa vile kuna kuwa na uhakika wa
chakula"anasema Khamis
Naibu waziri
Khamis anasema serikali itaendelea kuimarisha na kuendeleza juhudi za kulinda
Afya ya watoto kupitia unyonyeshaji maziwa ya mama, kutenga fedha na kufuatilia utekelezaji wa
sheria, kanuni na miongozo iliyopo .
Naibu waziri Khamisi anasema faida nyingine ya unyonyeshaji ni kuwajengea afya njema ambayo itawafanya wawe wenye mafanikio katika maisha yao nani chanzo bora cha virutubishi na kinga ya mwili.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464