Na Marco Maduhu, MWANZA
WANAHABARI hapa nchini, wametakiwa kujitoa kuandika habari ambazo zitasaidia kutatua matatizo ya jamii, na siyo kutanguliza pesa mbele.
Amesema Waandishi wa habari wanapaswa kuwa na moyo wa kujitoa (PASSION), katika kuandika habari zinazogusa maslahi ya jamii na kuzipata kipaumbele, zikiwamo za wachimbaji wadogo wa madini, ambao wanakabiliwa na matatizo mbalimbali yakiwamo matumizi ya Kemikali ya Zebaki ambayo ni hatari kiafya.
“Nawaombeni sana Waandishi wa habari muwe na shauku ya kufanya kazi ya kusaidia jamii na siyo kutanguliza pesa mbele, jitoleeni kuweni na Passion, na kusaidia pia hawa Wachimbaji wadogo wa Madini,”amesema Mhandisi Mwasha.
Aidha, amewataka pia Waandishi wa habari waandike mazuri ambayo wanayafanya wachimbaji wadogo wa madini, ikiwamo namna wanavyo changia pato la taifa.
Naye Afisa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Joseph Kiwango, akiwasilisha mpango kazi wa kupunguza matumizi ya Kemikali ya Zebaki kwa wachimbaji wadogo wa madini hapa nchini, amesema hadi kufikia mwaka 2025 matumizi hayo yawe yamepungua asilimia 30, na ifikapo 2030 Kemikali isitumike tena kukamatia dhahabu.
Amesema matumizi hayo ya Kemikali ya Zebaki yamekuwa na madhara makubwa kiafya kwa wachimbaji wadogo wa madini na jamii ambao inayowazunguka, na ndiyo maana Serikali mwaka (2020) iliridhia Mkataba wa Minamata kupunguza matumizi hayo ya Zebaki kwa wachimbaji wadogo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Jijini Mwanza (MPC) Edwin Soko, akizungumza kwa niaba ya Washiriki wa Semina hiyo, amewataka Wanahabari wayatumie mafunzo hayo kuandika habari ambazo zitakuza Sekta hiyo ya uchimbaji mdogo wa madini.
Katibu Mtendaji wa Taasisi ya kuendeleza Uchimbaji mdogo wa Madini FADev Mhandisi Theonestina Mwasha, akizungumza wakati akifunga Semina ya siku mbili kwa Wanahabari na Wahariri Kanda ya Ziwa.
Afisa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Joseph Kiwango, akizungumza kwenye Semina hiyo.
Afisa Program na utafiti kutoka FADev Evans Rubara akizungumza kwenye Semina hiyo.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Jijini Mwanza (MPC) Edwin Soko akitoa shukrani kwa niaba ya Washiriki wa Semina hiyo.
Washiriki wakiwa kwenye Semina.
Washiriki wakiwa kwenye Semina.
Washiriki wakiwa kwenye Semina.
Picha ya pamoja ikipigwa mara baada ya Semina hiyo kuhitimishwa leo Agosti 31 ambayo ilianza jana Agosti 30.