Zahanati ya kijiji cha Nyamigege halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga imekamilika.
Na Kareny
Masasy
SERA ya afya
ya mwaka 2007 inaeleza zahanati kujengwa umbali wa kilometa 5 za mduara na
kilometa 10 za mduara kwa kila kituo cha afya, hospitali katika kila wilaya,
mkoa na pia hospitali za rufaa na maalum.
Veronika
Swela na Shija Manhu wakazi wa kitongoji cha Isanagogo kijiji cha
Nyamigege kata ya Busangi halmashauri
ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga wanasema kuwa wamefurahi kupata Zahanati karibu wanajua
itaanza kufanya kazi nakupunguza safari
ndefu kufuata matibabu.
Swela
anasema kuwa Zahanati imekamilika
sasa wanachosubiri ni kupata wahudumu kwani walikuwa wakilazimika kusafiri kwa
pikipiki nakutumia gharama ya sh
10,000 kwenda na kurudi.
‘Tulikuwa tunateseka kukosa Zahanati karibu
ilibidi tutembee umbali wa kilomita kumi
kwenda Chela kituo cha afya au kilomita
8 kwenda Zahanati ya kijiji cha
Busangi kupata huduma ya kujifungua wakati mwingine ililazimu kujifungua njiani
au nyumbani”anasema Swela.
Mwenyekiti
wa kijiji cha Nyamigege Anthony
Guta anasema kuwa wananchi wamekuwa wakiteseka kutafuta huduma za afya
kwa kukosekana Zahanati karibu kwani wanatembea umbali mrefu licha ya
kuwepo Zahanati kijiji jirani pia hulazimika kwenda kituo cha afya
zaidi ya kilomita kumi kilichopo kata ya Chela.
“Mwaka 2011
walichanga wananchi kiasi cha sh
Millioni 12 na kuanzisha ujenzi wa jengo la Zahanati ambalo lilifikia hatua ya kuwekewa paa
na lilikaa muda mrefu bila kukamilishwa
na wazazi na wajawazito wanapata shida kupata huduma karibu za kliniki na
kujifungua”anasema Guta.
Diwani wa
kata ya hiyo Alexander Mihayo anasema kuwa kijiji hicho hakina Zahanati na huduma
za afya wanazipata vijiji vya jirani kwa kutembea umbali wa zaidi ya
kilomita tano na wengine kumi na
wajawazito kujifungulia wakati mwingine nyumbani.
“ Kijiji
hiki kina vitongoji vinne ambavyo ni Kisuke, Isanagogo, Bunangu na
Nyamigege ikiwa Zahanati hii ilianza kujengwa kwa nguvu za wananchi tangu
mwaka 2011 nakukamilisha hadi kuezeka paa”anasema Mihayo .
Mihayo
anasema kitu kilichokuwa kimebaki kuweka
ni saruji sakafuni na madirisha na vitu vingine na
hivyo waliachia halmashauri ikamilishe
na pindi ikikamilika wataweza
kuhudumia wakazi 3006 wa kijiji hicho”anasema Mihayo.
Mtendaji wa
kata hiyo Evamary Elias anasema kuwa kijiji cha Busangi ndiyo
kuna Zahanati ambayo kijiji cha Nyamigege wakazi wake ndiyo
wanakitegemea lakini kwa kutembea umbali wa zaidi ya kilomita tano wapo
wa mama wajawazito ambao walikuwa wakishindwa kwenda sababu
ya umbali mrefu nakujifungulia nyumbani.
“Wakazi wa
kijiji hiki kila mwaka walikuwa wakitoa kipaumbele chao katika upangaji wa
bajeti kuhusu Zahanati ikamilishwe na halmashauri tayari ilitenga bajeti kwa
mwaka wa fedha 2021/22 kiasi cha
shilingi millioni 50 ili kuweza kukamilisha
Zahanati hii”anasema Elias.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Mabao investment and general Pest
control Ltd ( AMJ) Abel Thomas imetoa msaada wa mifuko
ya saruji na giliri za madirisha kwa lengo
la ukamilishaji wa jengo la Zahanati na kuwaondolea adha ya
kutembea umbali mrefu kutafuta huduma ya afya maeneo ya vijiji jirani.
Mkurugenzi
wa Kampuni hiyo Abel Thomas anasema kuwa kuna jumla
ya mifuko 40 ya saruji na giri 25 za madirisha
nakugharamikia nguvu kazi ya ujenzi ikiwa vyote kwa pamoja vimegharimu zaidi ya shilingi Millioni 2.4.
Mganga mkuu wa halmashauri ya Msalala dkt Ernest Chacha anasema kuwa kuna vijiji 92 na tayari vijiji 30 vinazahanati na vituo vya afya vinne ambazo zinafanya kazi ya kutoa huduma na vijiji kumi vimekamilisha Zahanati zinasubiri kupata vifaa tiba na wataalamu kwaajili ya kutoa huduma.
“Kuna fedha
ambazo zimekuwa zikitolewa za huduma kwenye jamii (CSR) na mgodi wa Bulyanhulu ambazo ilitengwa bajeti yake kwa mwaka wa
fedha 2021/22 kiasi cha zaidi ya shilingi Billioni
1.245 na mpaka sasa kimetumika kiasi cha
zaidi ya shilingi Millioni 556.8.
Pia dk
Chacha anasema kuwa mapato ya ndani ya halmashauri bajeti ni Billioni 1.5 katika kutekeleza miradi ya afya ikiwemo
ujenzi wa Zahanati kupitia fedha hizo” anasema
dk Chacha.
Mbunge wa
jimbo la Msalala Kassimu Idd anasema kuwa serikali kuu imeleta fedha zaidi ya sh Billioni 2 katika sekta ya afya kwaajili ya ujenzi wa
majengo ya kutolea huduma mbalimbali pia imeleta wataalamu wa afya 56.