TBS YATOA ELIMU YA SAYANSI YA VIPIMO KWA WATAALAMU WA MAABARA SHINYANGA

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko  akizungumza wakati akifungua Semina ya Ufahamu juu ya elimu ya sayansi ya vipimo ‘Metrolojia’ wataalamu wa maabara za ubora na uchunguzi mkoa wa Shinyanga yaliyotolewa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS)
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko  akizungumza wakati akifungua Semina ya Ufahamu juu ya elimu ya sayansi ya vipimo ‘Metrolojia’ wataalamu wa maabara za ubora na uchunguzi mkoa wa Shinyanga yaliyotolewa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Shirika la Viwango Tanzania (Tanzania Bureau Standards- TBS) limeendesha Semina ya Ufahamu juu ya elimu ya sayansi ya vipimo ‘Metrolojia’ wataalamu wa maabara za ubora na uchunguzi mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya vipimo ili wafanye kazi kwa viwango na kutoa vipimo sahihi wanapofanya kazi zao.

Mafunzo hayo ya siku moja yakiongozwa na Kauli mbiu ya 'Sayansi ya Vipimo ni Ufunguo katika udhibiti Ubora - Metrology, key for Quality Control' yamefanyika leo Jumatatu Septemba 19,2022 katika ukumbi wa Manispaa ya Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema.

Akifungua mafunzo hayo, Mboneko amesema vipimo ni muhimu katika maisha ya binadamu hivyo kuwataka wataalamu wa vipimo kuzingatia ubora na kuwa na vipimo sahihi na kuyatumia mafunzo hayo kwenye taasisi zao kufanya upimaji wenye ubora na kuendana na ushindani wa kimataifa na kuleta tija kwa wateja wao.

“Tunaamini baada ya mafunzo haya vipimo vitakuwa bora, kutakuwa na takwimu sahihi ya vipimo. Tunategemea kuwa hatutaona tena utofauti wa vipimo. Mfano unakuta amepima kwenye kituo flani cha afya majibu yanakuwa tofauti na kituo kingine, unaweza kukuta unaumwa lakini vipimo vinaonesha hauumwi ukienda kupima kwingine unaibainika unaumwa…Hii hapana”,amesema Mboneko.

Amesema elimu ya sayansi ya vipimo 'Metrolojia' itaongeza ufanisi katika ufanyaji kazi na kutoa majibu yenye ubora kwa kuwa vifaa vinavyotumika kufanya vipimo tayari vimefanyiwa ugezi na kumpatia mpimwaji uhakika wa majibu yake huku akitaka vipimo sahihi kwenye maji yanayotumiwa na wananchi.

“Msiumbe umbe takwimu, msiunde unde matokeo ya vipimo mtaumiza wananchi. TBS watapita kwenye maeneo yenu ya kazi kukagua vipimo mnavyotumia, tunataka vipimo sahihi ili hata ukienda kwenye kituo kingine ukute matokeo/majibu yanafanana. Chukueni maamuzi ya kweli kwa kufanya vipimo sahihi ”,amesema Mkuu huyo wa wilaya.

Mboneko amesema uzalishaji wowote wenye tija na wa kibiashara au huduma inayokidhi vigezo vya ubora unaoweza kutambulika kitaifa na kimataifa ni lazima uzingatie viwango ambapo hatua ya kwanza katika kuzingatia ubora ni kuzingatia vipimo sahihi.

Aidha ameiomba TBS kuendelea kutoa mafunzo ya viwango kwa makundi mbalimbali ya wananchi wakiwemo wajasiriamali ili wazalishe kwa viwango huku akiwataka wajasiriamali kuthibitisha ubora wa bidhaa zao TBS.

“Tunaipongeza Menejimenti ya TBS kwa kukubali na kutenga bajeti ili kuwezesha semina hii kufanyika bila malipo yoyote kwa washiriki. Asanteni TBS kwa kutupa heshima Kanda ya Ziwa na hususani katika mkoa wetu wa Shinyanga”,amesema Mboneko.

Mboneko ameiomba TBS na Wamiliki wa bidhaa wawachukulie hatua wanaobadili muda wa matumizi ya bidhaa 'expiring dates' na kusababisha madhara kwa watumiaji huku akizitaka Halmashauri za wilaya kuendelea kufanya operesheni kwenye maduka kuondosha bidhaa zilizopitwa na wakati na wafanyabiashara wajali wateja kwa kuwapa bidhaa zenye ubora

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa upimaji na ugezi TBS, Mhandisi Johanes Maganga amesema TBS inatoa mafunzo ya Sayansi ya Vipimo ‘Metrolojia’ kwa ajili ya kusaidia taifa kuwa na vipimo sahihi.

Mhandisi Maganga ameeleza kuwa mafunzo hayo juu ya Sayansi ya Vipimo yamehusisha elimu kuhusu uelewa wa mifumo ya Metrolojia duniani na nchini, Majukumu na huduma ya Maabara ya Taifa ya Metrolojia na Matumizi ya Vyeti vya ugezi (Certificate of calibration).

Mhandisi Maganga amesema TBS wanavifanyia vifaa vya upimaji ugezi ili viweze kusoma na kutoa majibu sahihi na baadaye kutoa majibu ili kuthitisha ubora wa vipimo hivyo na baada ya mafunzo hayo watawatembelea kwenye maeneo yao ya kazi kuona ni namna gani wanavitumia vifaa vyao, na kueleza kuwa elimu ya vipimo inatakiwa kutolewa mara kwa mara.

“Tuna imani kuwa mara baada ya mafunzo haya, washiriki watafanya kazi kwa kuzingatia ubora na kuwa na vipimo sahihi. Mfanyakazi mbaya hulaumu vifaa vyake vya kazi, baada ya mafunzo haya hapatakuwa na mtu atakayelaumu vifaa vyake vya kazi”,ameongeza Mhandisi Maganga.

Akizungumzia kuhusu kazi za maabara ya Taifa ya Metrolojia, Mhandisi Maganga amesema ni pamoja na kutunza vipimo vya kitaifa,kutoa huduma ya unasabishaji wa vipimo,kutoa huduma ya ugezi, kuwakilisha nchi kimataifa katika masuala ya vipimo pamoja na kutoa mafunzo na ushauri katika masuala ya vipimo.

Meneja wa Metrolojia kutoka TBS, Stella Mroso amesema mafunzo hayo ya Metrolojia yameanza kutolewa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Mwanza, Kagera na Mara Septemba 6,2022 na yamehitimishwa mkoani Shinyanga Septemba 19,2022 yakihusisha wafanyakazi wa uzalishaji na upimaji katika viwanda, taasisi na wataalamu wa maabara kutoka hospitali.

“Lengo la mafunzo haya ni kuhakikisha tunafanya kazi zetu za vipimo kwa viwango na tuwe na vipimo sahihi. Mtoe vipimo kwa ubora ili kuwa na vipimo sahihi kwani vipimo sahihi vitatoa huduma bora”,amesema Mrosso.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko  akizungumza wakati akifungua Semina ya Ufahamu juu ya elimu ya sayansi ya vipimo ‘Metrolojia’ wataalamu wa maabara za ubora na uchunguzi mkoa wa Shinyanga yaliyotolewa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) leo Jumatatu Septemba 19,2022 katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko  akizungumza wakati akifungua Semina ya Ufahamu juu ya elimu ya sayansi ya vipimo ‘Metrolojia’ wataalamu wa maabara za ubora na uchunguzi mkoa wa Shinyanga yaliyotolewa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS)
Mkurugenzi wa upimaji na ugezi TBS, Mhandisi Johanes Maganga
akizungumza wakati wa Semina ya Ufahamu juu ya elimu ya sayansi ya vipimo ‘Metrolojia’ wataalamu wa maabara za ubora na uchunguzi mkoa wa Shinyanga yaliyotolewa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS)

Meneja wa Metrolojia kutoka TBS, Stella Mroso akizungumza wakati wa Semina ya Ufahamu juu ya elimu ya sayansi ya vipimo ‘Metrolojia’ wataalamu wa maabara za ubora na uchunguzi mkoa wa Shinyanga yaliyotolewa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS)

Wataalamu wa maabara za ubora na uchunguzi mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye Semina ya Ufahamu juu ya elimu ya sayansi ya vipimo ‘Metrolojia’  iliyoandaliwa  na Shirika la Viwango Tanzania (TBS)
Afisa Mwandamizi masuala ya Metrolojia TBS Joseph Kadenge akitoa Mada ya Mifumo ya Metrolojia 

Afisa kutoka TBS, Joseph Mahilla akitoa mada kuhusu Majukumu na huduma ya maabara ya taifa ya Metrolojia.

Afisa kutoka TBS, Adam Ziagi akitoa mada kuhusu Matumizi sahihi ya cheti cha ugezi 

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko  akipiga picha ya pamoja na wataalamu wa maabara za ubora na uchunguzi mkoa wa Shinyanga.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko  akipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wa TBS
Meneja wa Metrolojia kutoka TBS, Stella Mroso (kulia) akizungumza jambo na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464