. Mfanyabiashara maarufu wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro, James Mushi amefungua maombi madogo akiiomba Mahakama ya Wilaya hiyo itoe zuio la kusitisha usambazaji wa kadi na michango ya harusi ya mtu anayedaiwa kutumia jila lake na familia yake kuchangisha michango hiyo.
Akiwasilisha maombi hayo jana Jumatano Septemba 28, 2022,
wakili wa mfanyabiashara huyo, Elia Kiwia, mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa
mahakama hiyo, Julieth Mawole alidai mteja wake huyo ameingia kwenye mgogoro
mkubwa na familia yake na kutishia ndoa yake kuvunjika baada ya mke wake
kumtuhumu mumewe kuwa ni mzinifu.
"Kati ya tarehe 16 na 20, mwaka 2022 mteja wangu alipata
taarifa kuwa katika eneo la Boma ng'ombe, Machame na Arusha kuna mtu
alitengeneza kadi kwa ajili ya michango ya harusi na kusambaza kadi hizo za
mchango wa harusi kwa kutumia jina lake yeye na mke wake bila yeye
kushirikishwa," alisema
"Mheshimiwa kitendo hicho cha mtu huyo kutumia jina la
mlalamikaji yeye na familia yake imesababisha mgogoro mkubwa kwenye ndoa na
kuhatarisha ndoa yake kuvunjika.
“Ambapo mke wake mlalamikaji amemchukulia mume wake kama mtu mzinifu mwenye watoto nje ya ndoa kwa kumuingiza kwenye michango bila ridhaa yake" alieleza wakili Kiwia