DC MBONEKO AZINDUA VITABU VYA MIKAKATI YA KUBORESHA ELIMU, AONYA UDHALILISHAJI WALIMU

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizindua vitabu vitatu vya mikakati ya kuboresha elimu nchini katika Manispaa ya Shinyanga, (kulia) Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, (kushoto)Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Getrude Gisema.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA 

MKUU wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, amezindua vitabu vitatu vya mikakati ya kuboresha elimu nchini Manispaa ya Shinyanga, huku akionya wazazi kuacha mara moja tabia ya kudhalilisha walimu. 

Zoezi la uzinduzi wa vitabu vitatu vya mikakati ya kuboresha elimu, limefanyika leo Septemba 16, 2022 katika ukumbi wa mikutano kituo cha kulea watoto wenye mahitaji maalumu Buhangija, na kuhudhuliwa na wadau mbalimbali wa elimu wakiwamo na wakuu wa shule. 

Mboneko akizungumza kwenye uzinduzi huo wa vitabu, amesema vitabu hivyo vikatumike vizuri na kutekelezwa mikakati iliyokusudiwa ili kuboresha elimu na kupata ufaulu mzuri kwa wanafunzi na kutimiza ndoto zao na taifa kupata wataalamu wake. 

“Naombeni walimu vitabu hivi mkavisome na kuvielewa na siyo kwenda kuvifungia kwenye makabati, malengo ya Serikali ni kuona wanafunzi wote wanafanya vizuri kwenye masomo yao pamoja na kupata ufaulu mzuri,”amesema Mboneko. 

Aidha, Mboneko amesema katika suala la kuboresha elimu linatakiwa pia ushirikiano wa kutosha baina ya walimu na wazazi, na kukemea vitendo vya baadhi ya wazazi kudhalilisha walimu pamoja na wengine kuwapiga tena mbele ya wanafunzi. 

“Kwenye suala la kuboresha elimu wazazi na wao wanawajibu, sasa unakuta mazazi anaitwa na mwalimu shuleni kueleza matatizo ya mtoto wake akifika anaanza kumtolea lugha chafu mwalimu tena mbele ya wanafunzi, hilo sitaki tena kusikia,”amesema Mboneko. 

“Mwalimu mzazi akija shuleni na kuanza kukutukana, usimjibu weww kaa kimya nipeni taarifa halafu ataona namna nitakavyomshughulikia , tunataka heshima ya walimu irudi kama zamani, kwa sababu kazi ya walimu ni kubwa ndiyo inatoa viongozi na wataalamu mbalimbali hapa nchini,”ameongeza. 

Katika hatua nyingine, Mboneko amesema hataki kusikia suala la mwanafunzi wa kike wanabebeshwa ujauzito katika wilaya yake na kuagiza elimu ya afya ya uzazi itolewe kwa wanafunzi mara kwa mara pamoja na wanaume ambao hunyemelea wanafunzi wachukuliwe hatua. 

Pia amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya elimu hapa nchini, pamoja na kutoa kiasi cha fedha Sh. Bilioni 4.3 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Sekondari ya wasichana ambayo inajengwa Butengwa- Ndembezi Manispaa ya Shinyanga. 

Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, amewataka walimu wakavitumie vyema vitabu hivyo ambavyo vitawasaidia katika uboreshaji wa elimu huku akisema Serikali itaendelea kuboresha mazingira mazuri ya walimu kufundishia kupitia pia fedha za mapato ya ndani. 

Pia amewataka walimu wawe wanavaa nguo za staha, pamoja na kuacha ulevi wa kupindukia na matumizi ya lugha za mitaani,bali wajiheshimu ili kazi yao ipate kuheshimika pia. 

Naye Afisa elimu Sekondari Manispaa ya Shinyanga Lucas Mzungu, akizungumza kwenye uzinduzi wa vitabu hivyo amesema vimekuja kutatua changamoto zote ambazo zilikuwa zinaikabili Sekta ya elimu na vitaongeza ufaulu mkubwa kwa wanafunzi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza kwenye uzinduzi wa vitabu vitatu vya mikakati ya kuboresha elimu nchini katika Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza kwenye uzinduzi wa vitabu vitatu vya mikakati ya kuboresha elimu nchini katika Manispaa ya Shinyanga.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, akizungumza kwenye uzinduzi wa vitabu vitatu vya mikakati ya kuboresha elimu nchini katika Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa Kamati za huduma za jamii Manispaa ya Shinyanga Shela Mshandete, akizungumza kwenye uzinduzi wa vitabu vitatu vya mikakati ya kuboresha elimu nchini katika Manispaa ya Shinyanga.
Kaimu Mkurugenzi wa Mansipaa ya Shinyanga Getrude Gisema akizungumza kwenye uzinduzi wa vitabu vitatu vya mikakati ya kuboresha elimu nchini katika Manispaa ya Shinyanga.
Afisa elimu Sekondari Manispaa ya Shinyanga Lucas Mzungu, akizungumza kwenye uzinduzi wa vitabu vitatu vya mikakati ya kuboresha elimu nchini katika Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Mwasele Suzana Manoni, akizungumza kwenye uzinduzi wa vitabu vitatu vya mikakati ya kuboresha elimu nchini katika Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizindua vitatu vitatu vya mikakati ya kuboresha elimu nchini katika Manispaa ya Shinyanga, (kulia) Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, (kushoto)Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Getrude Gisema.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akionyesha vitatu vitatu vya mikakati ya kuboresha elimu nchini katika Manispaa ya Shinyanga mara baada ya kumaliza kuvizindua (kulia) Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, (kushoto)Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Getrude Gisema.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikaga vitabu vitatu vya mikakati ya kuboresha elimu kwa Wakuu wa Shule za Sekondari na Msingi Manispaa ya Shinyanga.
kuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikaga vitabu vitatu vya mikakati ya kuboresha elimu kwa Wakuu wa Shule za Sekondari na Msingi Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikaga vitabu vitatu vya mikakati ya kuboresha elimu kwa Wakuu wa Shule za Sekondari na Msingi Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikaga vitabu vitatu vya mikakati ya kuboresha elimu kwa Wakuu wa Shule za Sekondari na Msingi Manispaa ya Shinyanga.
Afisa elimu Sekondari Manispaa ya Shinyanga Lucas Mzungu, (kulia) akiwa na Afisa elimu Msingi Manispaa ya Shinyanga Neema Mkanga, kwenye uzinduzi wa vitabu vitatu vya mikakati ya kuboresha elimu.
Viongozi wakiwa kwenye uzinduzi wa vitabu vitatu vya mikakati ya kuboresha elimu.
Wadau wa elimu, wakuu wa shule na waratibu wa elimu, wakiwa kwenye uzinduzi wa vitatu vitatu vya mikakati ya kuboresha elimu nchini katika Manispaa ya Shinyanga.

Awali Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akisalimiana na viongozi wakati alipwasili kuzindua vitabu vitatu vya mikakati ya kuboresha elimu nchini katika Manispaa ya Shinyanga.
Awali Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akisalimiana na viongozi wakati alipwasili kuzindua vitabu vitatu vya mikakati ya kuboresha elimu nchini katika Manispaa ya Shinyanga.
Awali Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (kushoto) akiwa na Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, alipowasili kuzindua vitabu vitatu vya mikakati ya kuboresha elimu nchini katika Manispaa ya Shinyanga.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464